Mwenyekiti wa Usimamizi wa Ujenzi Soko la Utete Bw. Said Mkweya, akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya watendaji kutoka Ofisi ya Makamu wa pili wa RaisĀ wa Zanzibar na watendajiwa TASAF kutoka visiwani walipotembelea miradi TASAF wilayani Rufiji.
Pamela Bilukila Mratibu wa TASAF wilaya ya Rufiji akifafanua jambo Kwa watendaji kutoka Ofisi ya Makamu wa pili wa RaisĀ wa Zanzibar na watendajiwa TASAF kutoka visiwani walipotembelea miradi TASAF wilayani Rufiji.
Haji Kutoka Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais Serikali ya Mapinduzi ZANZIBAR akieleza jambo Kwa niaba ya wajumne wenzake baada ya kutembelea MRADI wa soko wilayani Rufiji.Baadhi ya wajumbe hao Kutoka Zanzibar wakiwa wakitembelea mradi wa soko Kata ya UTETE wilayani Rufiji.
Muonekano wa soko lililokengwa Kwa Fedha za TASAF kwenye Kata ya Utete wilayani Rufiji.
NA: JOHN BUKUKU, PWANI.
Mwananchi wa Kata ya Utete Wilaya ya Rufiki Mkoa wa Pwani wameushukuru Mfuko wa Maendeleo ya Jamii (TASAF) kwa kuwasaidia kuwapa fedha Shilingi milioni 127 kwa ajili ya ujenzi wa Soko kwani kwa muda mrefu walikosa eneo la kufanyia biashara.
Akizungumza na waandishi wa habari Mkoani Pwani.Ā Mei 30,2023 Mwenyekiti wa Usimamizi wa Ujenzi Soko la Utete Bw. Said Mkweya, amesema kuwa kabla ya ujenzi wa soko wananchi walikuwa wanapata shida kutokana na ukosefu wa soko katika eneo hilo.
Bw. Mkweya amesemaĀ hayo wakati akizungumza na waandishi wa habari baada ya ziara ya Watendaji kutoka Ofisi ya Makamu wa pili wa Rais Serikali ya Mapinduzi Zanzibar SMZ na watendajiwa wa TASAF kutoka visiwani humo wakati alipotembelea miradi TASAF inayotekelezwa Katika wilayani Rufiji.
Amesema uwepo wa soko utasaidia kuleta ahueni kwa wananchi kwani ni muhimu kwao katika kuhakikisha wanapiga hatua katika nyanja za maendeleo hasa kiuchumi
‘Tulikuwa na uhitaji wa soko kwa muda mrefu kupitia TASAF wakaona umuhimu wa kufanya na kuleta fedha kwa ajili ya ujenzi wa soko” amesema Bw. Mkweya.
Amefafanua katika kuhakikisha wanafikia lengo la ujenzi wa soko walifata kanuni na taratibu ikiwemo kuunda kamati kupitia mkutano wa wananchi.
Amesema kuwa waliunda kamati tatu ikiwemoĀ kamati ya ununuzi, ujenzi pamoja na mapokezi jambo ambalo limesaidia katika kufanikisha ujenzi huo.
“Baada ya fedha kutolewa kamati zote tulipewa mafunzo ya namna bora ya kusimamia ujenzi ili kufikia lengo la kukamilisha ujenzi wa soko hili utete” amesema.
Amesema kuwa licha ya uwepo wa changamoto mbalimbali walifanikiwa kutokana kamati zote zilikuwa zinaongea lugha moja katika utekelezaji wa majukumu katika kuhakikisha wanafikia lengo.