Home LOCAL MAKATIBU MAHSUSI TNZANIA WATAKIWA KUJIENDELEZA KIELIMU

MAKATIBU MAHSUSI TNZANIA WATAKIWA KUJIENDELEZA KIELIMU

Na: Tatyana Celestine

Makatibu Mahsusi Tanzania wameshauriwa kujiweka mahala wanapostahili Kitaaluma na kuondokanana kutoaminika mahala pa kazi ikiwa ni pamoja na kujiendeleza kielimu, kuwa waadilifu, kuongeza ufanisi na tija,kuwa wawazi pamoja na uwajibikaji.

Hayo yamesemwa na Mwalimu Charles Magaya ambaye ni mtoa mada muwezeshaji katika Mkutano wa 10 wa Kitaaluma wa Makatibu Mahsusi Tanzania unaoendelea mjini Zanzibar kwa lengo la kukumbushana wajibu na majukumu ya kazi kupitia mada isemayo Ufanisi wa Utendaji kazi wa Makatibu Mahsusi katika ofisi za umma.

Mwalimu Magaya amesema anaipongeza Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia Rais wa Awamu ya Sita Mhe. Samia Suluhu Hassan kwa kuwajali Makatibu Mahsusi katika kuwapa stahiki zao kikamilifu mahala pa kazi hivyo nao wahakikishe wanafanya kazi Kitaaluma ili kuonesha umuhimu wao mahala pa kazi.

Aidha Mwalimu Magaya ameongeza kuwa Kuna makundi matatu ya Makatibu Mahsusi na  kuyataja makundi hayo kuwa ni wale wanaofanya kazi kikamilifu, wanaofanya kazi wastani na wale ambao wamelegalega hivyo kuyataka makundi mawili ya mwisho yatumie Fursa hiyo kujifunza kupitia wanaofanya vizuri pamoja na kujiendeleza kielimu kwani anategemea mwaka ujao kuona wengi wao watakuwa wamejiendeleza na kujiunga na ngazi ya Shahada ambapo Sasa ni ruksa kwao.

Mkutano wa 10 wa Kitaaluma wa Makatibu Mahsusi Tanzania umeanza Mei 23, 2023 na utamalizika Mei 27 , 2023 ukiwa na kauli mbiu isemayo “Nidhamu,Uadilifu,na Utunzaji Siri sehemu za kazi ni Chachu ya Maendeleo Kitaaluma”.

Washiriki kutoka Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo (SUA) waliovaa share ya rangi ya kijani wakijumuika na Makatibu Mahsusi Tanzania katika Mkutano Mkuu wa Makatibu Mahsusi Tanzania unaofanyika mjini Zanzibar.

 

Previous articleWAHITIMU KIDATO CHA SITA 2023 WAITWA MAFUNZO YA JKT
Next articleMAHABUSU WALALAMIKIA VITENDO VYA RUSHWA MANYARA
Hughes Dugilo is a Writer, News Producer, Video-Photographer Journalist, and Video Editor experienced for 20 years now performing in News, Documentary, Advertisements and Television Programs. Aside from all above he own and operate his Blog known as Green Waves Media TZ since 2018.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here