Home SPORTS KMC YAIADHIBU SINGIDA BIG STARS 2-0

KMC YAIADHIBU SINGIDA BIG STARS 2-0

NA: TIMA SULTAN

KMC wameendeleza dhamira yao ya kushinda na kujiweka kwenye nafasi nzuri ya kumaliza Ligi Kuu ya NBC Tanzania Bara wakiwa kwenye nafasi nzuri kwakuhakikisha wanapata ushindi dhidi ya wageni wao Singida Big Stars

Wanakinondoni hao leo kwenye Uwanja wa Uhuru Jijini Dar es Salaam wamepata ushindi wa mabao 2_0 lakwanza lili ingizwa kimiani dakika ya 19 na Daruwesh Saliboko nakuiandikia timu yake KMC bao la ushindi akiunganisha pasi safi ya George Makang’a ambaye alikuwa karibu ya eneo la hatari.

Huku bao lapili likiwekwa kambani na Cliff Buyoya akipokea pasi nzuri kutoka kwa mchezaji Steve Nzigamasabo. Kipindi cha kwanza cha mchezo dakika ya sita Bright Ajei, anaambaa nampira kutika pembeneni lakini Ismail Gambo anakataa na inakuwa kona ambayo inachezwa na Bruno Gomez bila kuzaa matunda.

Dakika ya 14 KMC wanapata kona inachezwa na Kelvin Kijiri mpira unagonga kwenye ukuta wa Singida nakutua kwenye miguu ya Azizi Andambwile ambaye anapokonywa na wapinzani wake.

Dakika ya 19 Darwesh Saliboko anaindikia bao la kuongoza timu yake KMC akiunganisha pasi safi ya George Makang’a ambaye alikuwa karibu ya eneo la hatari.

Dakika ya 25 KMC wanaonekana kuutawala mchezo kumiliki mpira na kucheza pasi fupifupi wakiwasumbua wapinzani wao Singida Big Stars.

Dakika ya 34 Darwesh Saliboko anaambaa nampira kutoka upande wakushoto mwa uwanja anajaribu kushambulia lango la Singida na mpira inashindikana baada ya kuguswa na mchezaji mwingine.

Dakika ya 36 Bruno Gomez anacheza mpira wa adhabu kuelekea kuelekea KMC mpira unaguswa na wapinzani unakwenda nje inakuwa kona ambayo inachezwa na Gomez bila kuzaa matunda.

Abdul Majid Mangalo wa Singida anaonyeshwa kadi ya Njano dakika ya 38 kwakumfanyia madhambi Awesu Awesu.

Dakika ya 55 Singida wanafanya mabadiliko anatoka Paul Godfrey anaingia Deus Kaseke anatoka Bright Ajey anaingia Meddie Kagere wakati huo huo anaatoka Francis Kazadi anajngia Hamisi Tambwe raia wa Burundi.

Dakika ya 83 Anakwenda Benchi George Makanga wa upande wa KMC nakuingia Steve Nzigamasago nadakika hiyo hiyo Cliff Buyuyo anaindikia timu yake bao la pili akiunganisha pasi safii ya Steve ambaye ndio ameingia mchezoni.

Dakika ya 85 Golikipa Nurdin Balola anaonyeshwa kadi ya njano kwakupoteza muda wa mchezo .

Dakika 90+3 Zinamalizika kwa KMC kuondoka na pointi tatu za mchezo huo huku kwenye msimamo waligi hiyo wakisogea hadi nafasi ya 12 wakitoka kwenye ya 14 ambayo ingewalazimu kucheza Play Off.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here