Mwandishi Wetu
MTENDAJI Mkuu wa Mashindano Mnene Cup amezitaka klabu mbalimbali kujitokeza kwa wingi katika mashindano ya Mnene Cup ambayo yanatarajia kuanza kutimua vumbi Agosti Mosi mwaka huu.
Mashindano hayo yatakuwa chini ya Chama Cha Mpira wa Miguu wilaya ya Ilala(IDFA) ambao ndio wasimamizi wa mchezo huo.
Kauli hiyo ameitoa leo jana kwa waandishi wa Habari Jana Mtendaji Mkuu wa Mashindano hayo Saidi Ndege,amesema kuwa dirisha la usajili lilifunguliwa Mei Mosi na mwisho Juni 10 mwaka huu.
Ameongeza kuwa usajili huo utaenda sambamba na ulipaji wa ada za ushiriki kwa ajili ya gharama mbalimbali.
“Mashindano yetu tutaanzia kutafuta bingwa ngazi ya mtaa,kufuatia kata na baadaye wa Wilaya na lengo ni kuendeleza mpira na kuibua vipaji na vionekane na klabu zitakazoshiriki daraja la nne na tatu ,”alisema Ndege.
Alitaja zawadi za washindi bingwa ataondoka na kitita cha shilingi milioni mbili, na Kombe huku wa pili atapata milioni 1.5 na watatu atapata shilingi milioni moja.