Home LOCAL KADA WA CCM MAARUFU ‘TAI’ AKABIDHI OFISI YA CCM NYAMALOGO KUMUUNGA MKONO...

KADA WA CCM MAARUFU ‘TAI’ AKABIDHI OFISI YA CCM NYAMALOGO KUMUUNGA MKONO KWA VITENDO RAIS SAMIA

[

Muonekano wa sehemu ya jengo la Ofisi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) kata ya Nyamalogo katika Jimbo la Solwa Halmashauri ya Wilaya ya Shinyanga.

Na Kadama Malunde – Malunde 1 blog 
Kada wa Chama Cha Mapinduzi Titus Philipo Kalemela maarufu ‘TAI’ amekabidhi jengo la Ofisi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) kata ya Nyamalogo katika Jimbo la Solwa Halmashauri ya Wilaya ya Shinyanga ikiwa ni sehemu ya kumuunga mkono kwa vitendo Mwenyekiti wa CCM taifa ambaye ni Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan ili kurahisisha utendaji kazi wa shughuli za chama katika kata hiyo.

Hafla fupi ya makabidhiano ya jengo hilo la Ofisi ya CCM kata ya Nyamalogo ambalo ujenzi wake kuanzia boma, paa na madirisha vimetokana na fedha ya kada huyo wa CCM maarufu TAI imefanyika leo Ijumaa Mei 5,2023 ambapo mgeni rasmi alikuwa Katibu wa CCM Wilaya ya Shinyanga Vijijini Bi. Ernestina Richard.
 
Akizungumza wakati wa kukabidhi jengo la Ofisi ya CCM Kata ya Nyamalogo Titus Philipo Kalemela amesema sababu kuu iliyomsukuma kuchangia ujenzi huo ni kutokana na kukosekana kwa ofisi ya chama kwa muda mrefu katika kata hiyo.
 
“Mimi ni mzaliwa wa kata ya Nyamalogo, kama kada wa CCM nimeona njia bora ya kumuunga mkono Mwenyekiti wa CCM taifa ambaye ni Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan ni kujenga ofisi ya Chama ili kurahisisha shughuli za chama kata hii ikiwa ni pamoja na kutunza nyaraka za chama, kufanya vikao na shughuli zingine za kichama”,amesema Kalemela.
Kada wa Chama Cha Mapinduzi Titus Philipo Kalemela maarufu ‘TAI’ akishikana mkono na Katibu wa CCM Wilaya ya Shinyanga Vijijini Bi. Ernestina Richard (kulia) ishara ya kukabidhi jengo la Ofisi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) kata ya Nyamalogo katika Jimbo la Solwa Halmashauri ya Wilaya ya Shinyanga.
 
Akizungumza wakati wa kupokea jengo hilo, Katibu wa CCM Wilaya ya Shinyanga Vijijini Bi. Ernestina Richard amemshukuru na kumpongeza Titus Philipo Kalemela kwa uamuzi mzuri wa kuchangia ujenzi wa ofisi ya Chama.
 
“Jengo hili ni zuri sana. Ofisi hii ni nzuri na itakuwa na sehemu ya ukumbi wa vikao. Tunakushukuru sana ndugu yetu kwani ni watu wachache sana wanajitoa kujenga ofisi za Chama. Naomba ofisi hii itunzwe kwani itasaidia sana viongozi na Wanachama wetu kupata huduma hapa”,amesema Katibu huyo wa CCM.
 
Aidha ametumia fursa hiyo kuzihamasisha kata zingine pamoja na matawi kujenga ofisi za chama huku akisisitiza ofisi za CCM kuweka bendera za Chama pamoja na kuongeza wanachama.
 
Kwa upande wake Katibu wa Wazazi Wilaya ya Shinyanga Vijijini Hamis Salum na Katibu wa Siasa, Itikadi na Uenezi CCM Wilaya ya Shinyanga Vijijini Emmanuel Lukanda wamempongeza Titus Philipo Kalemela kwa uzalendo na moyo wake wa kujitolea kujenga ofisi ya chama wakisema huo ni mfano wa kuigwa.
Amewaomba viongozi wa Chama Cha Mapinduzi, Wanachama na wadau mbalimbali kuendelea kujitolea kukiunga mkono Chama Cha Mapinduzi kwa kushiriki kwenye shughuli za maendeleo huku akiomba waunge mkono katika hatua za umaliziaji ‘Finishing’ wa jengo la ofisi la CCM kata ya Nyamalogo.
 
Akitoa taarifa ya ujenzi wa ofisi ya CCM Kata ya Nyamalogo, Katibu wa CCM kata hiyo , Majilo Masanja amesema ujenzi huo unatokana na kikao cha Kamati ya siasa ya kata kilichofanyika Januari 23,2021 kilichokuwa na ajenda ya ujenzi wa ofisi ya kata awamu ya pili baada ya awamu ya kwanza iliyoanza mwaka 2013 kufeli.
 
“Kufuatia kikao hicho tulianza kukusanya michango na Januari 30,2023 ujenzi ulianza baada ya katibu wa CCM kata ya Nyamalogo kufanya mawasiliano na mdau Titus Philipo Kalemela ambapo siku hiyo hiyo alitoa mifuko 46 ya saruji. Hivyo mpaka sasa jengo hili limegharimu shilingi 6,841,700/= ambapo ndugu yetu Titus Kalemela ametuchangia zaidi ya shilingi Milioni 6 kwa ajili ya ujenzi wa boma, upauaji na madirisha na CCM kata ya Nyamalogo imechangia shilingi 848,000/= ”,ameeleza Masanja.
ANGALIA PICHA HAPA CHINI
Katibu wa CCM Wilaya ya Shinyanga Vijijini Bi. Ernestina Richard akizungumza leo Ijumaa Mei 5,2023 wakati wa hafla ya makabidhiano ya ofisi ya CCM kata ya Nyamalogo ambapo sehemu kubwa ya ujenzi huo imefadhiliwa na Kada wa Chama Cha Mapinduzi Titus Philipo Kalemela maarufu ‘TAI’. Picha na Kadama Malunde – Malunde 1 blog
Katibu wa CCM Wilaya ya Shinyanga Vijijini Bi. Ernestina Richard akizungumza leo Ijumaa Mei 5,2023 wakati wa hafla ya makabidhiano ya ofisi ya CCM kata ya Nyamalogo ambapo sehemu kubwa ya ujenzi huo imefadhiliwa na Kada wa Chama Cha Mapinduzi Titus Philipo Kalemela maarufu ‘TAI’

 Katibu wa CCM kata ya Nyamalogo , Majilo Masanja akitoa taarifa ya ujenzi wa ofisi ya CCM Kata ya Nyamalogo 
Katibu wa Siasa, Itikadi na Uenezi CCM Wilaya ya Shinyanga Vijijini Emmanuel Lukanda akizungumza wakati wa hafla ya makabidhiano ya jengo la Ofisi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) kata ya Nyamalogo katika Jimbo la Solwa Halmashauri ya Wilaya ya Shinyanga
Katibu wa Siasa, Itikadi na Uenezi CCM Wilaya ya Shinyanga Vijijini Emmanuel Lukanda (kulia) akimtambulisha Kada wa Chama Cha Mapinduzi Titus Philipo Kalemela maarufu ‘TAI’ wakati wa hafla ya makabidhiano ya jengo la Ofisi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) kata ya Nyamalogo katika Jimbo la Solwa Halmashauri ya Wilaya ya Shinyanga
Kada wa Chama Cha Mapinduzi Titus Philipo Kalemela maarufu ‘TAI’ akizungumza wakati akikabidhi jengo la Ofisi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) kata ya Nyamalogo katika Jimbo la Solwa Halmashauri ya Wilaya ya Shinyanga

Kada wa Chama Cha Mapinduzi Titus Philipo Kalemela maarufu ‘TAI’ akishikana mkono na Katibu wa CCM Wilaya ya Shinyanga Vijijini Bi. Ernestina Richard (kulia) ishara ya kukabidhi jengo la Ofisi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) kata ya Nyamalogo katika Jimbo la Solwa Halmashauri ya Wilaya ya Shinyanga
Viongozi wa CCM wakishikana mkono na Kada wa Chama Cha Mapinduzi Titus Philipo Kalemela maarufu ‘TAI’ wakati wa hafla ya kukabidhi jengo la Ofisi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) kata ya Nyamalogo katika Jimbo la Solwa Halmashauri ya Wilaya ya Shinyanga
Kada wa Chama Cha Mapinduzi Titus Philipo Kalemela maarufu ‘TAI’ akiwasalimia viongozi na wanachama wa CCM wakati wa hafla ya kukabidhi jengo la Ofisi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) kata ya Nyamalogo katika Jimbo la Solwa Halmashauri ya Wilaya ya Shinyanga
Katibu wa Wazazi Wilaya ya Shinyanga Vijijini Hamis Salum akizungumza wakati hafla ya kukabidhi jengo la Ofisi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) kata ya Nyamalogo katika Jimbo la Solwa Halmashauri ya Wilaya ya Shinyanga
Muonekano wa sehemu ya jengo la Ofisi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) kata ya Nyamalogo katika Jimbo la Solwa Halmashauri ya Wilaya ya Shinyanga
Muonekano wa sehemu ya jengo la Ofisi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) kata ya Nyamalogo katika Jimbo la Solwa Halmashauri ya Wilaya ya Shinyanga

Katibu wa CCM kata ya Nyamalogo , Majilo Masanja akionesha vyumba vya jengo la Ofisi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) kata ya Nyamalogo katika Jimbo la Solwa Halmashauri ya Wilaya ya Shinyanga
Katibu wa CCM Wilaya ya Shinyanga Vijijini Bi. Ernestina Richard (kulia) akiangalia jengo la Ofisi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) kata ya Nyamalogo katika Jimbo la Solwa Halmashauri ya Wilaya ya Shinyanga
Katibu wa CCM Wilaya ya Shinyanga Vijijini Bi. Ernestina Richard na viongozi mbalimbali wa CCM wakiangalia jengo la Ofisi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) kata ya Nyamalogo katika Jimbo la Solwa Halmashauri ya Wilaya ya Shinyanga

Mwenyekiti wa CCM kata ya Nyamalogo, Raphael Manota akizungumza wakati wa hafla ya kukabidhi jengo la Ofisi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) kata ya Nyamalogo katika Jimbo la Solwa Halmashauri ya Wilaya ya Shinyanga
Wananchi na wanachama wa CCM wakiwa kwenye hafla ya kukabidhi jengo la Ofisi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) kata ya Nyamalogo

Viongozi na wanachama wa CCM wakiwa kwenye hafla ya kukabidhi jengo la Ofisi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) kata ya Nyamalogo
Wananchi na wanachama wa CCM wakiwa kwenye hafla ya kukabidhi jengo la Ofisi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) kata ya Nyamalogo
 
Picha zote na Kadama Malunde – Malunde 1 blog
 
LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here