Makamu wa Rais Dkt. Philip Mpango (wa pili kushoto) akipata maelezao kutoka kwa Mkurugenzi wa wateja wadogo na binafsi wa benki ya NBC Elibariki Masuke (kulia) alipotembelea banda la benki hiyo wakati wa mkutano mkuu wa 37 wa Jumuiya ya Tawala za Mitaa Tanzania -ALAT unaofanyika jijini Arusha. Benki ya NBC ilikuwa ni mmoja wa wadhamini wa mkutano huo.
Mkurugenzi wa wateja wadogo na binafsi wa benki ya NBC Elibariki Masuke akitoa salamu za benki hiyo kama moja wa wadhamini wa mkutano mkuu wa 37 wa Jumuiya ya Tawala za Mitaa Tanzania -ALAT .Mkutano unafanyika ukumbi wa kimataifa wa mikutano wa AICC jijini Arusha.
Wafanyakazi wa benki ya NBC, wakiwa katika picha ya pamoja wakati wa mkutano mkuu wa 37 wa Jumuiya ya Tawala za Mitaa Tanzania -ALAT unaofanyika jijini Arusha. Benki ya NBC ilikuwa ni mmoja wa wadhamini wa mkutano huo.
Arusha, Mei 29, 2023
Makamu wa Rais Dkt. Phillip Mpango ameipongeza Benki ya Taifa ya Biashara (NBC) kwa kuendelea kusaidia mamlaka za serikali za mitaa nchini na kwa gawio walilotoa kwa serikali na kuwasii wafanye bidii zaidi ili kuweza kuchangia zaidi pato la serikali kwa ajili ya maendeleo ya nchi.
Dkt. Mpango alitoa wito huo wakati alipotembela banda la benki hiyo katika
Mkutano Mkuu wa 37 Jumuia ya Tawala za Mitaa Tanzania (ALAT) unaoendelea jijini Arusha. NBC Bank ilikuwa miongoni mwa wadhamini wa mkutano huo ambao ulifunguliwa rasmi na Makamu wa Rais.
Akizungumza na uongozi wa benki hiyo, Dkt. Mpango alipongeza benki hiyo kwa kuendelea kusaidia miradi inayolenga kuzisaida mamlaka za serikali za mitaa na kukuza maendeleo katika ngazi ya msingi.
“Napongeza hatua nzuri ya NBC kufikia kiwango cha kutoa huduma jumuishi, lakini bado ninaendelea kusisitiza dhamira ya serikali kuendelea na mipango mkakati ya kutoa huduma za kifedha nafuu ili watanzania wengi waweze kufaidi. Wito huu nautoa kwa taasisi za kifedha zote nchini ili ziweze kusaidia Watanzania kadiri iwezekanavyo lengo likiwa ni kuwawezesha waweze kuongeza mitaji wao na kuunda uchumi jumuishi.” Alisisitiza.
Kwa upande wake, Elibariki Masuke, Mkurugenzi wa Biashara za reja reja wa benki ya NBC ambaye alimwakilisha Mkurugenzi Mtendaji wa benki hiyo, alionyesha kuridhishwa na uwepo wa uhusiano mzuri kati ya benki hiyo na ALAT huku akiahidi kuendelea kushirikiana na jumuiya hiyo katika jitihada zake za kukuza utawala bora na maendeleo nchini. Pia alionyesha matumaini kuhusu uwezekano wa ushirikiano zaidi kati ya taasisi hizo mbili.
“Tunafurahi kupokea sifa kama hizi na wito kutoka kwa Makamu wa Rais Dkt. Philip Mpango. Tunatambua pia kazi nzuri za mamlaka za serikali za mitaa katika kuongoza maendeleo ya kiuchumi ya nchi yetu. Kazi yao nzuri imeendelea kuwanufaisha Watanzania wengi. Kama benki inayotumikia vizuri taifa letu, Benki ya NBC tunaahidi kusaidia na kutoa suluhisho la kibenki linalotokana na mahitaji.” Aliongeza.
Masuke alisema benki hiyo pia ni miongoni mwa walipa kodi wakubwa waliochangia zaidi ya TZS 66.5 bilioni kwenye hazina ya taifa mwaka kwa 2022.
Katika kipindi hicho hicho, Benki ililipa gawio la serikali lenye thamani ya bilioni 6 TZS. “Tuna furaha kuwa mshirika muhimu na mshiriki katika ajenda ya maendeleo ya kitaifa, na tunahakikisha kuendelea kusaidia. Milango yetu inaendelea kuwa wazi ili kutumikia si tu serikali na watumishi wa umma lakini Watanzania wote kwa ujumla.”
Benki ya NBC inatoa huduma mbalimbali za kielektroniki kwa Halmashauri za Wilaya na Miji katika ukusanyaji wa mapato na suluhisho za malipo ambayo yanapunguza gharama za kifedha.
Uwezo huu unaimarishwa zaidi na mfumo wake wa malipo ya Serikali, mtandao wake mkubwa wa NBC Wakala, mashine za POS, na usimamizi wenye usalama katika malipo na ukusanyaji kwa rahisi zaidi.
Benki hiyo hivi karibuni ilizindua huduma yake kibenki ya kidigitali inayofahamika kama “NBC Connect” ambayo pamoja na mambo mengine inalenga kurahisisha malipo kwa njia mtandao. Benki hito pia inatoa huduma mbalimbali za mikopo ili kukidhi mahitaji ya taasisi, makampuni, na watu binafsi.
“Zaidi tunaendelea kuhusika katika miradi muhimu ya serikali ili kuongoza maendeleo ya kiuchumi ukiwemo mradi wa ujenzi wa reli ya SGR. Pia tumekuwa tukisaidia vikundi maalum kama wajasiriamali, mnyororo wa thamani ya kilimo, AMCOS, Wamachinga, bodaboda, na makundi mengine,” Masuke alisema.
Mwisho .