Home LOCAL DIWANI AIDANI KWEZI KUPANDA MITI ELFU 20,000 KIPAWA ILALA

DIWANI AIDANI KWEZI KUPANDA MITI ELFU 20,000 KIPAWA ILALA

Na: Heri Shaaban (Ilala)

Diwani wa Kata ya Kipawa Wilayani Ilala Aidani Kwezi amesema Kata ya Kipawa inatarajia kupanda miti Elfu 20,000 ya vivuli na matunda Mwaka huu 2023

Diwani Aidani Kwezi aliyasema hayo wakati wa uzinduzi wa Kampeni ya SOMA na MTI ambayo imezinduliwa katika shule 16 za Msingi na Sekondari walizopanda miti 2000 Kata ya Kipawa Wilayani Ilala .

“Kampeni ya SOMA na MTI ambayo imezinduliwa Leo Kata ya Kipawa itakuwa endelevu dhumuni letu katika kata ya Kipawa kupanda Miti Elfu 20,000 ya vivuli na matunda itakuwa endelevu kwa ushirikiano na Wananchi wangu” alisema Aidani.

Diwani Aidani Kwezi alisema mikakati yake kila kaya kupanda miti mitano ya matunda na kivuli Ili iweze kusaidia vizazi vijavyo katika Taifa Ili .

Aliwapongeza Walimu wa shule za Msingi na Sekondari kuungana mkono juhudi za Serikali katika Kampeni hiyo ya utunzaji wa mazingira na kuakikisha shule zote zinakuwa na miti .

Aliwataka Wanafunzi wa shule hizo wawe mabalozi wa Mazingira kwa kusoma na Mti Ili waweze kutambua suala zima la utunzaji wa mazingira kwani miti ina kazi nyingi kwa Jamii na Taifa kwa ujumla ikiwemo kuifadhi vyanzo vya maji ,utunza Mazingira na kuifanya nchi isigeuke kuwa jangwa .

Akizungumzia Sekta ya Elimu alipongeza Walimu wa Kipawa kufanya vizuri katika Taaluma aliwataka Wazazi kushirikiana na Walimu kwa ajili ya kufatilia maendeleo ya watoto wao shuleni .

Alitumia nafasi hiyo kumpongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan, kuwekeza katika sekta elimu msingi na elimu sekondari pamoja na miradi mikubwa ya Maendeleo ikiwemo sekta ya afya,miundombinu ya Barabara na Reli ya kisasa SGR .

Diwani wa Viti Maalum Wanawake Wilaya ya Ilala Magreth Cheka, aliwapongeza Walimu wa shule za Kipawa kwa ushirikiano wao Kwa kukuza taaluma shuleni katika sekta ya Elimu na kuwataka waendelee kuisaidia Serikali kwani kazi yao ni wito .

Afisa Elimu Taaluma Halmashauri ya Jiji Magdalena Mandia, alipongeza Kampeni ya SOMA na MTI mashuleni na kuwataka Walimu kutoa elimu ya Mti mashuleni na umuhimu wake.

Mwisho.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here