Home LOCAL DC CHATO AIPONGEZA RUWASA UTEKELEZAJI MIRADI YA MAJI

DC CHATO AIPONGEZA RUWASA UTEKELEZAJI MIRADI YA MAJI

Mkuu wa wilaya ya Chato Mkoani Geita Deusdetis Katwale Amewapongeza Wakala wa Maji na Usafi wa Mazingira Vijijini RUWASA Wilaya ya Chato kwa utekelezaji mzuri wa miradi ya maji katika wilaya hiyo.

Katwale amesema hayo katika Mkutano Mkuu wa mwaka wa vyombo vya watumia maji ngazi ya jamii (CBWSO’s) pamoja na wadau wa sekta ya maji wilayani chato amesema serikali imejipanga vyema kuhakikisha wananchi wote wanafikiwa na huduma ya maji hasa wanaoishi maeneo ya vijijini.

Amesema RUWASA Wilaya ya chato wanafanya kazi nzuri hivyo amewaomba kuongeza kasi ya utekelezaji wa miundombinu ya maji kwa lengo la kuhakikisha wananchi wote wanapata maji katika wilaya hiyo ili kuwawezesha kuondokana na changamoto ya kukosa maji safi na salama katika maeneo yao.

Meneja wa Wakala wa Maji na Usafi wa Mazingira Vijiji RUWASA wilaya Ya chato Mhandisi Avitus Exavery amesema katika wilaya hiyo wanahudumia kata 19 zenye wakazi zaidi ya laki 487,000 huku hali ya upatikanaji wa maji vijijini katika wilaya hiyo imefikia asilimia 68.

Mhandisi Avitus amesema kwa sasa wanaendelea na utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maji katika wilaya hiyo huku kwa mwaka wa fedha ujao 2023/24 wilaya ya chato imepangiwa zaidi ya bilioni 4.3 kwa ajili ya kuendelea kutekeleza miradi ya maji katika wilaya hiyo.

Amesema RUWASA pamoja na kujenga miradi ya maji wanajukumu kubwa la kuhakikisha huduma ya maji inakuwa endelevu Katika ngazi za jamii hivyo wameamua kutoa Pikipiki 7, Bajaji moja na Kompyuta mbili kwa vyombo vya watoa huduma ya maji ngazi ya jamii (CBWSO’s) zenye thamani ya zaidi ya milioni 30 ili kuboresha huduma kwa wasimamizi wa miradi ya maji ngazi ya jamii.

Nao baadhi ya wakazi wa wilaya ya chato pamoja na wadau mbalimbali wa maji wilayani humo wameipongeza RUWASA wilaya ya chato kwa utekelezaji wake wa miradi ya maji kwani kwa sasa wanapata maji safi na salama kwa urahisi zaidi huku wakiondokana na changamoto za kukosa huduma ya maji safi na salama katika maeneo yao.

Previous articleWAZIRI MCHENGERWA AIPONGEZA BENKI YA CRDB KWA KUTOA MSAADA WA PIKIPIKI KWA JESHI LA POLISI KUIMARISHA USALAMA KWA WATALII JIJINI ARUSHA
Next articleKAYA 10,000 ZANUFAIKA NA TASAF WILAYANI SAME
Hughes Dugilo is a Writer, News Producer, Video-Photographer Journalist, and Video Editor experienced for 20 years now performing in News, Documentary, Advertisements and Television Programs. Aside from all above he own and operate his Blog known as Green Waves Media TZ since 2018.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here