Home LOCAL DART: TUNAWAHITAJI ZAIDI MADEREVA WANAWAKE KWA SABABU YA UMAKINI WAO KAZINI

DART: TUNAWAHITAJI ZAIDI MADEREVA WANAWAKE KWA SABABU YA UMAKINI WAO KAZINI

NA: JOHN BUKUKU, DODOMA

Wanawake nchini wametakiwa kuchangamkia fursa kwa kusoma kozi ya udereva (Class C) ili waweze kuajiriwa na Wakala wa Mabasi Yaendayo Haraka (DART) kwani wameonekana kuwa makini katika utekelezaji wa majukumu yao ya kuendesha magari yaendayo haraka bila kusababisha uharibifu wowote.

Akizungumza leo mwishoni mwa wiki Mkoani Dodoma katika semina maalam ya kuwajengea uwezo waandishi habari, Meneja wa Mipango na Usafirishaji Wakala wa Mabasi Yaendayo Haraka (DART) Mhandisi Mohamed Kuganda, alisema kuwa DART imefanikiwa kuajiri madereva 360 kati yao wanawake 18.

Mhandisi Kuganda alisema kuwa madereva wanawake 18 ambao wamefanikiwa kufanya nao kazi katika kuendesha magari yaendayo haraka wapo makini na kuwa tofauti na wanaume.

“Tuna madereva wanawake 18 na wapo makini sana kwani hawajawahi kusababisha ajali katika utekelezaji wa wanajukumu yao barabarani wakati wanaendesha magari yaendayo haraka, ajali nyingi  za DART zimesababishwa na madereva wanaume “ alisema Mhandisi Kuganda.

Mhandisi Kuganda alisema kuwa madereva wengi wanawake wapo makini katika kuendesha magari kutokana  na kuwa na nidhamu Katika kazi  na  wanafanya kwa uweledi mkubwa mpaka abiria wanafurahia.

Alisema kuwa madereva wanapaswa kuwa na nidhamu katika kuendesha magari ili kuepukana na ajali ambazo asilimia kubwa zinasababishwa na madereva wasiokuwa makini.

“Tunaomba wazazi waweze kuwapeleka vijana wao wa kike kusoma fani ya udereva, Kwa sababu sisi kama DART  tuna uhitaji mkubwa  wa madereva na kwa sababu wanawake wapo makini na kazi tunawahitaji sana” amesema Mhandisi Kuganda.

Amebainisha kuwa katika kuhakikisha wanaongeza idadi ya madereva wa kike wamekuwa na programu maalam ya kuwajengea uwezo madereva wa kike 100 iliyofanyika katika Chuo Cha Usafirishaji Tanzania (NIT).

“Kati ya madereva wanawake 100 ambao tuliwajengea uwezo ni madereva 18 walifanikiwa kujiunga na Kwa Sasa wanafanya kazi na DART wengine waliendelea kufanya kazi katika Kampuni na taasisi nyengine za usafirishaji” amesema Mhandisi Kuganda.

Previous articleCCM YATOA TAARIFA YA KIKAO CHA KAMATI KUU,YAMPONGEZA MWENYEKITI WAKE
Next articleMAGAZETI YA LEO JUMATATU MEI 22 , 2023
Hughes Dugilo is a Writer, News Producer, Video-Photographer Journalist, and Video Editor experienced for 20 years now performing in News, Documentary, Advertisements and Television Programs. Aside from all above he own and operate his Blog known as Green Waves Media TZ since 2018.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here