Home LOCAL DANIEL KALINAKI ACHAGULIWA RAIS JUMUIYA YA WAHARIRI AFRIKA MASHARIKI

DANIEL KALINAKI ACHAGULIWA RAIS JUMUIYA YA WAHARIRI AFRIKA MASHARIKI

JUMUIYA ya Wahariri Afrika Mashariki imemchagua Daniel Kalinaki wa Jukwaa la Wahariri Uganda kuwa Rais wa Jumuiya ya Wahariri Afrika Mashariki kuanzia Mei 12, 2023, ambapo ataongoza kwa mwaka mmoja.

Deodatus Balile, ambaye ni Mwenyekiti wa Jukwaa la Wahariri Tanzania (TEF), naye amechaguliwa kuwa Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wahariri Afrika Mashariki, kuanzia Mei, 2024 hadi Mei, 2025.

Kwa mujibu wa Katiba ya Jumuiya ya Wahariri Afrika Mashariki, katika kipindi cha mwaka mmoja ambacho Balile anasubiri kushika wadhifa wa Urais wa Jumuiya ya Wahariri Afrika Mashariki mwezi Mei 2024, kwa sasa atakuwa ni Naibu Rais wa Jumuiya ya Wahariri ya Afrika Mashariki.

Umoja wa Wahariri wa Afrika Mashariki Katiba yake inatoa nafasi ya kumwandaa kiongozi wake ajaye kwa mwaka mmoja baada ya kumchagua kama sehemu ya maandalizi ya kuifahamu vyema kazi yake kabla ya kushika madaraka hayo rasmi.

Previous articleRAIS SAMIA AFANYA UTEUZI
Next articleMAGAZETI YA LEO JUMAMOSI MEI 13,2023
Hughes Dugilo is a Writer, News Producer, Video-Photographer Journalist, and Video Editor experienced for 20 years now performing in News, Documentary, Advertisements and Television Programs. Aside from all above he own and operate his Blog known as Green Waves Media TZ since 2018.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here