Home LOCAL COMRED CHONGOLO ATOA MAAGIZO WIZARA YA KILIMO

COMRED CHONGOLO ATOA MAAGIZO WIZARA YA KILIMO

IRINGA

Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Daniel Chongolo amemuagiza Waziri wa Kilimo Hussein Bashe kuhakikisha ndani ya Wiki tatu anafika katika kata ya Masaka iliyopo kwenye halmashauri ya Wilaya ya Iringa akiwa ameambatana na timu ya Wataalamu kutoka Wizarani kwake kwa ajili ya kuangalia namna ya kujenga skimu ya umwagiliaji itakayokuwa na tija kwa Wakulima wa eneo hilo.

Komredi Chongolo ametoa agizo hilo Leo Mei 29, 2023 baada ya kuzindua upandaji wa samaki katika mradi wa Bwawa la Masaka, ikiwa ni sehemu ya ziara yake ya siku 7 Mkoani Iringa.

Maelekezo ya Katibu mkuu wa (CCM) Chongolo kwa Waziri wa Kilimo Hussein Bashe yanakuja kufuatia Malalamiko ya Diwani wa Kata ya Masaka Mathew Nganyagwa kudai tume ya taifa imeshindwa kufika kwenye kata hiyo ili kuweka mifereji ya maji kwenye mabwawa kwa ajili ya kuimarisha Shughuli za Kilimo katika Ukanda huo.

“Mimi wala sipigi kelele kwa Sababu umeshasema, najua wale mabwana wanajua wajibu wao, ninakwenda kuzungumza na Waziri wao wa Kilimo ili watafute pesa ya Kujenga Skimu ya Umwagiliaji katika eneo la Upande wa pili kwa Sababu tayari maji yapo” amesema Chongolo.

Bwawa la Kisaka lina ukubwa wa kilomita za mraba 5.33, huku likitarajia kunufaisha Wananchi zaidi ya Elfu Kumi wanaopatikana ndani na nje ya Kata ya Masaka iliyopo Halmashauri ya Wilaya ya Iringa.

Previous articleYASEMAVYO MAGAZETI YA LEO JUMANNE MEI 30-2023
Next articleMBUNGE KABATI: WANAWAKE TUSHIKAMANE KUMUUNGA MKONO DKT. SAMIA
Hughes Dugilo is a Writer, News Producer, Video-Photographer Journalist, and Video Editor experienced for 20 years now performing in News, Documentary, Advertisements and Television Programs. Aside from all above he own and operate his Blog known as Green Waves Media TZ since 2018.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here