Home Uncategorized CHONGOLO AKERWA HALI YA UDUMAVU WILAYA YA MUFINDI | AHIMIZA VITA DHIDI...

CHONGOLO AKERWA HALI YA UDUMAVU WILAYA YA MUFINDI | AHIMIZA VITA DHIDI YA VVU

Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Daniel Chongolo amesema hali ya udumavu katika Wilaya ya Mufindi bado ni tatizo kubwa licha ya wilaya hiyo kuwa ni wazalishaji wa mazao mbali ya Chakula na Biashara.

Chongolo amesema hayo wilayani Mafinga mkoani Iringa wakati alipokuwa akizungumza na makundi mbalimbali ya Kijamii wakati wa ziara yake yenye lengo la Kukagua Utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya CCM.

Kufuatia Changamoto ya Udumavu kwa Watoto, Chongolo ameyahimiza makundi hayo ya Kijamii kuhamasisha ulaji wa chakula bora ili kuondoa tatizo hilo kwa wakazi wa wilaya hiyo, ambapo amesema bila kufanya hivyo ni vigumu kupata nguvu kazi itakayokuwa na uwezo wa kuzalisha mali kwa ajili ya maendeleo ya Wilaya hiyo.

Katika hatua nyingine Katibu Mkuu Daniel Chongolo amewakumbusha viongozi wa Wilaya hiyo kuendelea kutoa elimu kuhusu maambukizi ya virusi vya ukimwi kwa kuwa mufindi takwimu zinaonyesha bado maambukizi yako juu.

Ziara ya Katibu mkuu huyo wa CCM inaendelea mkoani Iringa akiwa ameambatana na Katibu NEC itikadi na Uenezi Sophia Mjema pamoja na Katibu wa NEC Oganaizesheni Issa Haji Gavu.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here