Home LOCAL BERNALD MEMBE AFARIKI DUNIA

BERNALD MEMBE AFARIKI DUNIA

Aliyewahi kuwa Waziri wa Mambo ya Nje wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Bernard Kamilius Membe, amefariki Dunia muda mfupi uliopita katika Hospitali ya Kairuki Jijini Dar es Salaam.
Taarifa za awali kutoka kwa watu wake wa karibu zinasema kuwa, Membe alipata changamoto ya kifua na kupelewa Hospitalini hapo alfajir ya leo Mei 12 na baadaye kuaga Dunia.
Itakumbukwa kuwa Bernard Membe aliwahi kugombea kiti cha Urais kupitia tiketi ya Chama cha ACT Wazalendo katika uchaguzi Mkuu wa mwaka 2020.
Mwenyezi Mungu ailaze Roho ya Bernard Membe mahala pema Peponi. AMEN

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here