Home LOCAL ACHENI KUFANYA SHUGHULI ZA KIBINADAMU NDANI YA HIFADHI YA VYANZO VYA MAJI

ACHENI KUFANYA SHUGHULI ZA KIBINADAMU NDANI YA HIFADHI YA VYANZO VYA MAJI

NA: FARIDA MANGUBE, MOROGORO

Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa Mwaka 2023 Abdalla Shaib Kaim amewataka Wakazi wa Manispaa ya Morogoro hasa wanaishi karibu na Bwawa la Mindu kuacha kufanya shughuli za kibinadamu ndani ya Mita Mia 5 ya Bwawa Hilo.

Ameyasema hayo wakati alipo ongoza zoezi la kupanda miti katika Bwawa la Mindu ambapo amesema kufanya shughuli za kibinadamu karibu na vyanzo maji kunachochea uharibufu wa Mazingira.

“Niwatake Wakazi wa Manispaa ya Morogoro kuacha kufanya shughuli za kibinadamu karibu na vyanzo vya Maji kama kukata miti, kulima na ufugaji kwenye vyanzo vya Maji.” Alisema Kiongozi wa mbio za Mwenge Kitaifa Mwaka 2023.

Akisoma Taarifa ya Mradi wa kupanda miti Bwawa la Mindu Afisa rasilimali Maji Bodi ya maji Bonde la Wami – Ruvu Martin Kasambala amesema mradi huo imeghalimu shilingi Milioni 50.

Amesema Mradi huo ni sehemu ya utekelezaji wa agizo la Makamu wa Rais DKt. Philipo Mpango la kupanda miti Milioni moja na laki tano (2, 000, 000) kila kila Mwaka.

Pia Katika kuendeleza uhifadhi Katika vyanzo vya Maji Wami – Ruvu imeadhisha kitalu cha miche ya miti ya aina mbalimbali ikiwemo matunda na kugawa kwa wakazi walio karibu na vyanzo vya Maji.

Bwawa la Mindu ni miongoni mwa vyanzo Maji zaidi ya 231 vilivyo chini ya Bodi ya maji Bonde la Wami -Ruvu lenye uwezo wa kuhifadhi Mita za ujazo 12. 6 na kutegemewakwa asilimia 75 na wakazi wa Manispaa ya Morogoro kwa Maji.

Mwenge wa Uhuru mwaka 2023 ukiwa Manispaa ya Morogoro umetembelea, kukagua, kuweka jiwe la Msingi na kuzindua Miradi 14 yenye thamani ya zaidi ya Shilingi Bil. 1.

Previous articleUVCCM ZANZIBAR: YASEMA UWEKEZAJI WA SMZ KATIKA SEKTA YA MICHEZO NI FURSA KWA VIJANA
Next articleWIZARA YA AFYA YAKAMILISHA MAJENGO YA HUDUMA ZA DHARURA
Hughes Dugilo is a Writer, News Producer, Video-Photographer Journalist, and Video Editor experienced for 20 years now performing in News, Documentary, Advertisements and Television Programs. Aside from all above he own and operate his Blog known as Green Waves Media TZ since 2018.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here