Home LOCAL TMDA: MAONI YA WADAU YATASAIDIA KUBORESHA MIFUMO YA USAJIRI 

TMDA: MAONI YA WADAU YATASAIDIA KUBORESHA MIFUMO YA USAJIRI 

Dkt.Yona Mwalwisi Mkurugenzi wa Dawa za binadamu na Mifugo Mamlaka ya Dawa na Vifaa Tiba TMDA akifungua kikao kazi Cha Wadau na Mamlaka hiyo kilichokutana kwenye Hoteli ya Holliday Inn jijini Dar es Salaam ili kujadiliana kuhusu changamoto na mafanikio ya wafamasia kwenye majukumu Yao ya Kila siku.

Dkt.Yona Mwalwisi Mkurugenzi wa Dawa za binadamu na Mifugo Mamlaka ya Dawa na Vifaa Tiba TMDA akifungua kikao kazi Cha Wadau na Mamlaka hiyo kilichokutana kwenye Hoteli ya Holliday Inn jijini Dar es Salaam ili kujadiliana kuhusu changamoto na mafanikio ya wafamasia kwenye majukumu Yao ya Kila siku, kulia ni Mhadhiri wa Chu Kikuu  Cha Sayansi ya na Sayansi Shirikisho (MUHAS) Dkt. Betty Maganda

Gaudensia Simwanza, Meneja Mawasiliano na Elimu kwa Umma kutoka Mamlaka ya Dawa na Vifaa tiba (TMDA) akifafanua jambo Katika kikao kazi hicho.

Dkt.Yona Mwalwisi Mkurugenzi wa Dawa za binadamu na Mifugo Mamlaka ya Dawa na Vifaa Tiba TMDA akifurahia jambo wakati Mhadhiri wa Chu Kikuu  Cha Sayansi ya na Sayansi Shirikisho (MUHAS) Betty Maganda akizungumza.

NA: MWANDISHI WETU, DAR

MAMLAKA ya Dawa na Vifaa Tiba (TMDA) imekutana na wadau wa Dawa nchini ikiwemo waigizaji wa dawa na vifaa tiba katika kupata mrejesho wa pande zote namna bora ya usajili wa Dawa pamoja na Dawa zinazoingia nchini.

Akizungumza leo  jijini Dar es Salaam katika warsha hiyo ya wadau hao ya kujadili kwa kina changamoto zinazohusiana na usajili wa dawa, Mkurugenzi wa Dawa za Binadamu na Wanyama, TMDA, Yona Mwalwisi amesema wanategemea kupata maoni ya wadau, ili waweze kuboresha huduma.

“Tumekutanisha wadau wa famasi, hospitali ambao ni watumiaji wa dawa tunategemea na kupata maoni ya vifaa tiba pia ni mkutano muhimu kwa mamlaka, kwani tutapokea maoni ambayo yatasaidia kuboresha mifumo yetu ya usajili, uingizaji na usafirishaji wa dawa nje ya nchi,” amesisitiza.

Amesema warsha hiyo ni muhimu pia katika kutoa mrejesho kwa wadau wao kwa sehemu ambazo hawajaenda vizuri, kwani kuna vitu wanatakiwa watekeleze, hivyo mkutano unatoa nafasi kwa pande zote mbili namna ya kuboresha huduma.

“Suala la dawa na vifaa tiba walengwa ni wagonjwa kama mamlaka tunataka kuhakikisha mgonjwa ambaye anatumia bidhaa hizo apate bidhaa bora, salama na fanisi lengo ni kuendelea kumlinda Mtanzania,” ameeleza.

Mwalwisi amesema watatumia nafasi hiyo kuwaelimisha sheria na taratibu za dawa ili wawalinde wananchi.

“Kwenye upande wa uingizaji kikubwa ni kuzingatia sheria na taratibu za uingizaji kulingana na vigezo tunavyohitaji,” amesema.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here