Na: Mwandishi wetu
KIKOSI cha KMC leo wameibuka na ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Singida Big Stars katika mchezo wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara uliochezwa katika Uwanja wa Uhuru Jijini Dar es Salaam.
Katika mchezo huo mabao ya KMC yamefungwa na Daruwesh Saliboko dakika ya 20 na Cliff Buyoya dakika ya 84.
Hata kwa ushindi huo wanafikisha pointi 29 na kusogea nafasi ya 12, huku kwa upande Singida Big Stars wamejikusanyia jumla ya alama 51 nafasi ya nne wakiwa wamecheza mechi 28.