Home LOCAL ZIARA YA KATIBU MKUU WA CHAMA CHA MAPINDUZI KOMREDI DANIEL CHONGOLO KATIKA...

ZIARA YA KATIBU MKUU WA CHAMA CHA MAPINDUZI KOMREDI DANIEL CHONGOLO KATIKA JAMHURI YA WATU WA CHINA

Katibu wa (NEC) Itikadi na Uenezi Ndg. Sophia Mjema akizungumza na Waandishi wa Vyombo vya habari(hawapo pichani) akiwasilisha taarifa ya ziara ya Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi, Ndg. Daniel Godfrey Chongolo, pamoja na ujumbe wake (Waliosimama nyuma ) katika ziara ya Kikazi na Mafunzo nchini China,walio ,Ofisi ndogo ya CCM Lumumba mara baada ya Kuwasili Nchini Leo April 28,2023.

Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi, Ndg. Daniel Godfrey Chongolo, pamoja na ujumbe wake Tarehe 17 hadi 28 Aprili, 2023 amefanya Ziara ya Kikazi na Mafunzo nchini China, ambapo walitembelea majimbo matatu (3) ikiwemo Beijing, Hebei, na Guandong.

Ziara hii ni Utekelezaji wa Makubaliano na Maelekezo yaliyotolewa na Viongozi Wakuu Dkt. Samia Suluhu Hassan, Mwenyekiti wa CCM na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Komredi Xi Jinping Katibu Mkuu wa CPC na Rais wa Jamhuri ya Watu wa China.

Viongozi Wakuu walikubaliana kupandisha hadhi ya Uhusiano kati ya CCM na CPC kwa upande mmoja na kati ya Tanzania na China kwa upande mwingine, kuwa na uhusiano maalum wa kimkakati katika nyanja za Elimu na Ufundi stadi, Habari na Mawasiliano, Kilimo, Uvuvi, Afya na Viwanda.

Tunamshukuru sana Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kufungua milango ya mahusiano na ushirikiano kimataifa.

Katika ziara yake nchini China, Katibu Mkuu na Ujumbe wake alikutana na kufanya mazungumzo na viongozi mbalimbali wa Chama cha Kikomunisti cha China na Serikali ya Jamhuri ya Watu wa China ambao ni Komredi Wang Yi, Mkurugenzi wa Kamisheni ya Mambo ya Nje wa Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China, Komredi Liu Jianchao, Waziri wa Idara ya Mambo ya Nje ya Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China Komredi Li Mingxiang, Naibu Waziri wa Idara ya Mambo ya Nje ya Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China, Komredi Ni Yuefeng, Katibu wa Chama cha Kikomunisti cha China Jimbo la Hebei na Komredi Wang Ruijun, Mjumbe wa Kamati ya Kudumu ya Chama cha Kikomunisti cha China Jimbo la Guandong.

Katika mazungumzo hayo, viongozi wa pande zote mbili walikubaliana haja ya kuendelea kuchagiza na kudumisha uhusiano katika nyanja mbalimbali kwa maslahi ya vyama vyetu, na wananchi wa  nchi zetu mbili.

Chama kimejifunza na kuona jinsi wenzao walivyoweza kufungua nchi zao kupitia majimbo ya Shengzen, Guandong na Guanzhou. Kwa kuwakaribisha wawekezaji na kufanya kazi kwa pamoja. dhana inayoendana na dhana ya Katibu Mkuu wa CPC Xi Jingping ya “The Belt and Road initiative (BRI)” ya kuja kufungua uchumi Afrika. 

Ziara hii imekuwa ya muhimu sana katika kuboresha na kuimarisha mahusiano kati ya CCM na CPC na kati ya Tanzania na China.

Nitumie fursa hii kuwashukuru wenzetu wa China kwa  mapokezi mazuri na ukarimu wao waliouonesha wakati wote kwa Ujumbe wa CCM nchini humo. Mwisho nitoe rai kwa wanachama na viongozi wa CCM na Watanzania wote kuchangamkia fursa zitokanazo na matunda ya ziara hii.

KIDUMU CHAMA CHA MAPINDUZI

KIDUMU CHAMA CHA KIKOMUNISTI CHA CHINA

UDUMU UHUSIANO MWEMA WA TANZANIA NA CHINA

Previous articlePSSSF YAPITA “BANDA KWA BANDA” KUWAFIKIA WANACHAMA WAKE KWENYE MAOENSHO YA SIKU YA KIMATAIFA YA USALAMA NA AFYA MAHALI PA KAZI
Next articleWCF YATWAA TUZO SIKU YA KIMATAIFA YA USALAMA NA AFYA MAHALI PA KAZI
Hughes Dugilo is a Writer, News Producer, Video-Photographer Journalist, and Video Editor experienced for 20 years now performing in News, Documentary, Advertisements and Television Programs. Aside from all above he own and operate his Blog known as Green Waves Media TZ since 2018.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here