Home LOCAL WAZIRI MKUU AFUTURISHA MAKUNDI YA WATU MBALIMBALI RUANGWA

WAZIRI MKUU AFUTURISHA MAKUNDI YA WATU MBALIMBALI RUANGWA

Mbunge wa Jimbo la Ruangwa na Waziri Mkuu Kassim Majaliwa Aprili 17, 2023 ameshiriki katika futari na baadhi ya wakazi wa Wilaya ya Ruangwa, Lindi.

Akizungumza wakati wa Iftari hiyo Mheshimiwa Majaliwa amewataka viongozi wa Dini waendelee kuliombea Taifa pamoja na viongozi wakuu wote ili Tanzania iendelee kuwa kimbilio la mataifa mengine yanayokosa amani

“Nchi hii inapendwa sana na mwenyezi Mungu, Mwenyezi Mungu anaupendo mkubwa na Tanzania, kwa uwepo wa dini zote na kazi kubwa mnayoifanya ndio neema tunayoina sasa, huu utulivu ni wenu”

Kadhalika Waziri Mkuu amewataka wananchi kuendelea kuzingatia mafundisho ya dini na kufuata wanachoasa viongozi wa dini ili kulifanya Taifa liendelee kuwa na amani

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here