Home LOCAL WATOA HUDUMA WA AFYA NGAZI YA JAMII WAWEZESHWA KUWAIBUA WENYE TRAKOMA NA...

WATOA HUDUMA WA AFYA NGAZI YA JAMII WAWEZESHWA KUWAIBUA WENYE TRAKOMA NA MTOTO WA JICHO

Meneja Mradi wa Shirika la Hellen Keller International Bw. Athuman Tawakal akieleza namna wanavyowafundisha wahudumu wa afya ngazi ya jamii kuwaibua watu wenye matatizo ya Vikope(Trakoma) na Mtoto wa Jicho ili kuzuia uoni unaozuilika.

Mhudumu wa afya ngazi ya jamii Bw. Wilbroad Mkwama kutoka kijiji cha Mpola akielezea namna walivyonufaika na mafunzo hayo na namna wanavyoweza kuwapima watu wenye matatizo ya mtoto wa jicho.

Muonekano wa hospitali ya Wilaya ya Mbarali ambapo kambi ya upasuaji wa mtoto wa jicho inafanyika hapo.

Na: WAF, Mbarali

Zaidi ya watoa huduma wa afya ngazi ya jamii 3000 wa mikoa ya Njombe, Mbeya, Songwe,Iringa na Manyara wamejengewa uelewa wa kuwatambua wagonjwa wa Vikope(Trakoma) na mtoto wa jicho na hivyo kuwasaidia wananchi kuondoa uoni unaoweza kutibika

Hayo yameelezwa na Meneja Mradi kutoka Shirika la Hellen Keller International la nchini hapa Bw. Athuman Tawakal kwenye kambi ya upasuaji wa mtoto wa jicho unaofanyika katika hospitali ya wilaya ya Mbarali.

Bw. Tawakal amesema kuwa njia hiyo imesaidia sana kuhakikisha kwamba wanawafikia jamii kwa asilimia kubwa kwani wahudumu hao wanatoka kwenye jamii zao.

“Tunahakikisha tunawafundisha wahudumu ngazi ya jamii na baadae kupita kaya kwa kaya jambo ambalo limesaidia wananchi kuhakikisha wanajikinga na uoni unaoweza kuzuilika”.

Ameongeza kuwa njia hiyo ya kuwafundisha wahuduma ngazi ya jamii kutoka kila kitongoji imesaidia kuwabaini wenye matatizo na hivyo wataalamu huweza kufika na kuwathibitisha wagonjwa na baadae kuandaa kambi za upasuaji bila malipo.

Aidha, Bw. Tawakali ameipongeza Serikali kwa kuboresha miundombinu kwenye hospitali nchini zikiwemo zile za wilaya na kuongeza kuwa kwa mara ya kwanza wameweza kufanya upasuaji katika ‘theater’ ya hospitali ya Mbarali.

Naye, Mhudumu wa afya ngazi ya jamii Bw. Wilbroad Mkwama kutoka kijiji cha Mpolo amesema muitikio wa wananchi katika kaya umekua ni mkubwa na hivyo kuweza kuwaibua wagonjwa.

Kuhusu mafunzo waliyoyapata Bw. Mkwama amesema wameyafurahia kwani wananchi wamekua wakiwapigia simu hata kama wanaumwa macho ya kawaida na kuwashauri kufika kwenye vituo vya kutolea huduma za afya.

Previous articleRAIS SAMIA ATENGUA UTEUZI WA MKURUGENZI WA JIJI LA MWANZA 
Next articleWANACHUO MZUMBE WAPATIWA ELIMU YA MILIKI UBUNIFU
Hughes Dugilo is a Writer, News Producer, Video-Photographer Journalist, and Video Editor experienced for 20 years now performing in News, Documentary, Advertisements and Television Programs. Aside from all above he own and operate his Blog known as Green Waves Media TZ since 2018.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here