Home LOCAL WANANCHI NYANG’HWALE WAFURAHIA HUDUMA YA MAJI.

WANANCHI NYANG’HWALE WAFURAHIA HUDUMA YA MAJI.

Meneja wa RUWASA wilaya ya Nyang’hwale Mhandisi Moses Mwampunga.

Meneja wa RUWASA Mkoa wa Geita Mhandisi Jabiri Kayilla

Na: Costantine James, Geita

Wakazi wa wilaya ya Nyang’hwale Mkoani Geita wameishukuru serikali kupitia kwa Wakala wa Maji na Usafi wa Mazingira Vijijini (RUWASA) wilayani humo kwa kutatua changamoto ya ukosefu wa maji safi na salama iliyokuwa ikiwakabili kwa mda mrefu.

Wananchi hao wameeleza namna walivyokuwa wanapata changamoto yakufata maji umbali mrefu huku maji hayo yakiwa sio safi na salama pamoja na kusababisha ndoa zao kuteteleka kutokana na wakina mama kutumia mda mrefu kutafuta maji.

Wamemshukuru Mhe. Rais Samia Suluhu kwa kuwawezesha kutatua changamoto hiyo na sasa wanapata kwa urahisi zaidi huku wakiepukana na magojwa ya mara kwa mara yaliyokuwa yanasababishwa na matumizi ya maji yasiyo salama.

Meneja wa RUWASA wilaya ya nyang’hwale Mhandisi Moses Mwampunga amesema mwaka 2020 hali ya upatikanaji wa maji katika wilaya hiyo ilikuwa ni asilimia 24 lakini kwa sasa hali ya upatikanaji wa waji umeongezeka kutoka asalimia 26 hadi kufikia asilimi 64.5.

Amesema miradi zaidi ya saba imekamilika na wananchi wanapata huduma ya maji huku wakiendelea na utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maji kwa lengo la kuongeza wigo wa upatikanaji wa maji kutoka asilimia 64.5 hadi kufikia asilimia 85.

Meneja wa RUWASA mkoa wa Geita Mhandisi Jabiri Kayilla amesema RUWASA mkoa wa Geita inaendelea kutekeleza miradi mbalimbali ya maji katika wilaya hiyo kwa lengo la kuwawezesha wananchi kupata huduma hiyo kwenye maeneo yao.

Mhandisi Kayilla amewataka wakazi wa wilaya hiyo kuitunza miradi ya maji pamoja na kuwa walinzi wa kwanza kwenye miradi hiyo ili iweze kutumika kwa mada mrefu kwani serikali inatumia pesa kubwa kutekeleza miradi ya maji.

Previous articleWANAOHUJUMU MIUNDOMBINU MRADI WA SGR KUKAMATWA
Next articleMAHAFALI YA KIDATO CHA SITA NATTA SEKONDARI YAFANA, WAJIPANGA KUFANYA VIZURI MITIHANI YA KITAIFA
Hughes Dugilo is a Writer, News Producer, Video-Photographer Journalist, and Video Editor experienced for 20 years now performing in News, Documentary, Advertisements and Television Programs. Aside from all above he own and operate his Blog known as Green Waves Media TZ since 2018.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here