Home BUSINESS WANACHUO MZUMBE WAPATIWA ELIMU YA MILIKI UBUNIFU

WANACHUO MZUMBE WAPATIWA ELIMU YA MILIKI UBUNIFU

Wakala wa Usajili wa Biashara na Leseni BRELA inaendesha mafunzo katika vyuo mbalimbali jijini Mbeya ili kuongeza uelewa kuhusu Miliki Ubunifu.

Akizungumza katika Mafunzo hayo leo tarehe 18 Aprili, 2023 katika Chuo Kikuu cha Mzumbe Jijini Mbeya, Afisa Sheria kutoka BRELA Bw. Abdulkarim Nzori amesema Bunifu mbalimbali zikitumiwa zinaweza kutatua changamoto katika jamii na kuwakuza kiuchumi wabunifu na wafanyabiashara.

Katika mafunzo hayo yaliyohudhuriwa na wanafunzi zaidi ya 1000, wameelekezwa namna wanavyo weza tumia bunifu zao kujikwamua kiuchumi na kutengeneza ajira kwa watu wengine.

Wanafunzi hao pia wamepata fursa ya kukumbushwa kuwa Miliki Ubunifu ni mali inayotokana na mtu kutumia akili kubuni vitu mbalimbali hivyo wabunifu na wafanyabiashara wanayo nafasi kutumia bunifu zao kama vile Alama za Biashara na Huduma zilizosajiliwa BRELA kutambulisha bidhaa au huduma wanazitoa na wanaweza kuziuza au kuzikodisha Alama hizo pale inapobidi hivyo kunufaika na bunifu zao.

Awali akitoa neno la utangulizi Afisa Sheria kutoka BRELA Bi. Grace Umoti amewahamasisha wanafunzi hao kuchangamkia fursa ya ufadhili wa masomo ya Shahada ya Uzamili katika fani ya Miliki Ubunifu inayotolewa na BRELA pindi nafasi hizo zinapotangazwa ili kujiongezea ujuzi na kupanua wigo wa watalamu katika nyanja ya Miliki Ubunifu

Maafisa wa BRELA wanaendelea kutoa Mafunzo katika Vyuo Vikuu na vyuo vya Mafunzo ya ufundi stadi (VETA) na Shirika la Kuhudumia viwanda vidogo (SIDO) katika Jiji la Mbeya

Previous articleWATOA HUDUMA WA AFYA NGAZI YA JAMII WAWEZESHWA KUWAIBUA WENYE TRAKOMA NA MTOTO WA JICHO
Next articleDAWASA YAANZA SHAMRASHAMRA ZA MUUNGANO, UHIFADHI MAZINGIRA WAENDELEA KUPEWA KIPAUMBELE
Hughes Dugilo is a Writer, News Producer, Video-Photographer Journalist, and Video Editor experienced for 20 years now performing in News, Documentary, Advertisements and Television Programs. Aside from all above he own and operate his Blog known as Green Waves Media TZ since 2018.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here