Home Uncategorized WAKAZI WA DAR ES SALAAM CHUKUENI TAHADHARI YA KIPINDUPINDU;UMMY MWALIMU

WAKAZI WA DAR ES SALAAM CHUKUENI TAHADHARI YA KIPINDUPINDU;UMMY MWALIMU

Na. WAF – Dar es Salaam

Waziri wa Afya Mhe. Ummy Mwalimu amewataka wananchi kuchukua tahadhari juu ya uwepo wa mlipuko wa ugonjwa wa Kipindupindu Jijini Dar es Salaam.

Waziri Ummy ameyasema hayo leo baada ya kutoa taarifa juu ya hali ya ugonjwa wa Marburg mbele ya waandishi wa habari katika ofisi ndogo za Wizara ya Afya, Jijini Dar es Salaam.

“Mlipuko huu wa Kipindupindu mhisiwa alitokea katika Kata ya Kivule wilaya ya Ilala tarehe 16 Aprili 2023 Jijini Dar es Salaam.” amesema Waziri Ummy

Ameendelea kubainisha kuwa hadi kufikia tarehe 28 Aprili 2023 wagonjwa 15 waliotolewa taarifa (wagonjwa 13 walitoka Wilaya ya Ilala na wagonjwa 2 Kinondoni).

Aidha, Waziri Ummy amesema kati ya wagonjwa 15, wagonjwa 13 wamepona kwa kuwa waliwahi katika vituo vya kutolea huduma za afya huku wagonjwa wawili waliobakia wanaendelea na matibabu na hali zao zinaendelea vizuri.

“Nitoe wito kwa Watanzania tutibu maji kwa kutumia dawa ya Chlorine au kuchemsha maji ya kunywa na kuhakikisha upatikanaji wa maji salama.” amesema Waziri Ummy

Pia, kuepuka uchafuzi wa maji, kuepuka kula chakula kilichopoa, pia kunawa mikono kwa sabuni na maji tiririka, kuosha matunda kwa maji safi kabla ya kuyala.

Watu wote wanaotiririsha maji taka kutoka chooni waache mara moja kwakuwa kumekuwa na baadhi ya watu wenye nia ovu na hili tutalisimamia vyema.” amesema Waziri Ummy

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here