Home BUSINESS WAFANYABIASHARA WATAKIWA KUCHANGAMKIA FURSA SOKO HURU AFRIKA

WAFANYABIASHARA WATAKIWA KUCHANGAMKIA FURSA SOKO HURU AFRIKA

Serikali yawataka wafanyabiashara kuchangamkia fursa za biashara na uwekezaji zilizopo katika eneo huru la biashara Afrika kupitia mkataba wa (AfCTA).

Hayo yamebainishwa katika kikao cha pamoja kati ya Wizara ya Uwekezaji, Viwanda na Biashara na wafanyabiashara pamoja na wadau mbalimbali waliokutana hivi karibuni jijini Dar es Salaam.

Kaimu Mkurugenzi wa kitengo cha utengamano wa biashara, Wizara ya Uwekezaji, Viwanda na Biashara, Bw. Ombeni Mwasha amesema lengo la kikao hicho ni kuelimishana kuhusu fursa mbalimbali za biashara na uwekezaji zilizopo katika eneo huru la biashara Afrika pamoja kuwaeleza  masharti na vigezo ambavyo wanapaswa kuvifuata watakapoanza kupeleka biadhaa katika  soko hilo.

Aidha Mwasha amesema Mkataba  wa eneo huru la biashara Afrika (AfCTA) una maeneo mengi ya ushirikiano na unafursa mbalimbali za kibiashara, masoko na uwekezaji.

Kwa kutambua fursa hizi Serikali iliridhia mkataba huu Januria 2022, hivyo sasa jukumu letu kubwa ni kujipanga ili wafanyabiashara wetu waweze kwenda kuuza bidhaa zao kwenye soko hili.

Aliongeza kusema zipo bidhaa nyingi ambazo tunaweza kuuza kwenye soko hilo ikiwemo biadhaa  za kilimo, mifungo, uvuvi ambazo zinapaswa kuongezewa thamani na kuzipeleka katika soko.

Kwa upande wake Afisa Biashara Mkuu Wizara ya Uwekezaji, Viwanda na Biashara, Bi. Sekela Mwaisela amesema soko huru la Africa ni soko kubwa  kwa kuwa bara hilo linakadiriwa kuwa  na wakazi  bilioni 1.3  hivyo amewataka wafanyabiashara na wazalishaji kuchangamkia soko hilo na pia kuzalisha kwa kuzingatia viwango vya ubora vilivyokubalika.

Bi. Mwaisela aliongeza kusema Tanzania ni moja ya nchi saba zilizoteuliwa kufanya majaribio ya soko hili hivyo wameanza kwa kutoa warsha na makongamano kwa wafanyabiashara kuwaelezea namna ya kufanya biashara ndani ya Afrika.

Amesema, Tanzania ina fursa kubwa katika biashara ya mazao ya kilimo hasa  chakula. Tanzania tunaweza kulisha Afrika kwa kuangalia ukanda wa SADC, EAC kote watu wanahitaji chakula, hata ukiangalia katika takwimu utaona jinsi nchi yetu inavyouza mazao ya chakula.

Alisisitiza kuwa  ili bidhaa iuzwe katika soko hilo inahitajika iwe inayotoka ndani ya Afrika, unaweza kuchukua malighafi kutoka nchi yoyote ya Afrika na kuiongezea thamani na kwenda kuuza biadhaa inakubalika, lakini si kununua kutoka nje ya Afrika na kuiza hiyo haikubaliki.

Kwa upande wake Afisa anayeshughulikia masoko ya ndani na nje ya nchi kutoka  Chemba ya Wafanya Biashara, Wenye Viwanda na Kilimo Tanzania (TCCIA) Bi. Josephine Moshi amewataka wafanyabiashara kuzingatia kuwa na cheti cha Uasili wa Bidhaa kwa kuwa kitamsadia mfanyabiashara kutokuchajiwa ushuru katika nchi ambayo ni mwanachama wa soko hilo, alisema hiyo itamsaidia  mfanyabishara husika kuweza kuuza kwa bei ya ushindani katika soko.

Bi. Mosha alisema cheti cha uasilia kinatolewa kwa biashara kubwa na  ndogo ambapo wanyabiashara walio na mtaji chini ya dola elfu cheti cha uasili kinatolewa mipakani na TRA na kwa aliye na mtaji kuanzia elfu dola elfu mbili na ziada inatolewa na TCCIA.

Naye mmiliki wa kiwanda cha kutengeza kahawa mumunyifu, Amir Hamza ameipongeza wizara kwa kuwapa warsha hii kwani baada ya kusikia kuhusu soko huru la biashara itawasaidia kuuza biadhaa zao katika sehemu kubwa Afrika.

Ni mfumo mzuri utakapokamilika utakuwa ni msahada mkubwa kwetu, kwani kupitia soko hili unaweza kuingiza biadhaa katika nchi mbalimbali bila ya kupata vikwazo vya kodi kubwa na ushuru ambao awali ilikuwa kikwazo.” Alisema Hamza.

 

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here