Home Uncategorized WABUNIFU WAMSHANGAZA RC DODOMA KATIKA WIKI YA UBUNIFU 2023 UWANJA WA JAMHU

WABUNIFU WAMSHANGAZA RC DODOMA KATIKA WIKI YA UBUNIFU 2023 UWANJA WA JAMHU

Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Bi.Rosemary Senyamule,akipata maelezo kutoka kwa Meneja Uhusiano VETA Bw.Sitta Peter mara baada ya kutembelea banda la VETA wakati wa  Maonyesho ya Wiki ya Ubunifu 2023 inayowakutanisha wabunifu mbalimbali kutoka ndani na nje ya nchi yaliyoandaliwa na Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia yaliyoanza Aprili 24 hadi 28 mwaka huu  katika uwanja wa Jamhuri Jijini Dodoma.

Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Bi.Rosemary Senyamule,akisaini kitabu cha wageni  mara baada ya kutembelea banda la VETA wakati wa  Maonyesho ya Wiki ya Ubunifu 2023 inayowakutanisha wabunifu mbalimbali kutoka ndani na nje ya nchi yaliyoandaliwa na Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia yaliyoanza Aprili 24 hadi 28 mwaka huu  katika uwanja wa Jamhuri Jijini Dodoma.

Wanafunzi na wananchi mbalimbali wakipata maelezo katika  banda la VETA wakati wa  Maonyesho ya Wiki ya Ubunifu 2023 inayowakutanisha wabunifu mbalimbali kutoka ndani na nje ya nchi yaliyoandaliwa na Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia yaliyoanza Aprili 24 hadi 28 mwaka huu  katika uwanja wa Jamhuri Jijini Dodoma.

   

Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Bi.Rosemary Senyamule,akisaini kitabu cha wageni  mara baada ya kutembelea banda la VETA wakati wa  Maonyesho ya Wiki ya Ubunifu 2023 inayowakutanisha wabunifu mbalimbali kutoka ndani na nje ya nchi yaliyoandaliwa na Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia yaliyoanza Aprili 24 hadi 28 mwaka huu  katika uwanja wa Jamhuri Jijini Dodoma.

Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Bi.Rosemary Senyamule,akiwa ndani ya gari akiendeshwa na wanafunzi waliobuni gari mara baada ya kutembelea  Maonyesho ya Wiki ya Ubunifu 2023 inayowakutanisha wabunifu mbalimbali kutoka ndani na nje ya nchi yaliyoandaliwa na Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia yaliyoanza Aprili 24 hadi 28 mwaka huu  katika uwanja wa Jamhuri Jijini Dodoma.

Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Bi.Rosemary Senyamule,akizungumza na washiriki wa maonyesho (hawapo pichani)  mara baada ya kutembelea na kukagua  Maonyesho ya Wiki ya Ubunifu 2023 inayowakutanisha wabunifu mbalimbali kutoka ndani na nje ya nchi yaliyoandaliwa na Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia yaliyoanza Aprili 24 hadi 28 mwaka huu  katika uwanja wa Jamhuri Jijini Dodoma.

Mkurugenzi wa Mafunzo ya Ufundi Stadi -VETA  Ndg.Abdallah Ngodu,akielezea bunifu zinazofanywa na VETA katika Maonyesho ya Wiki ya Ubunifu 2023 inayowakutanisha wabunifu mbalimbali kutoka ndani na nje ya nchi yaliyoandaliwa na Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia yaliyoanza Aprili 24 hadi 28 mwaka huu  katika uwanja wa Jamhuri Jijini Dodoma.

Mkurugenzi wa Sayansi, Teknolojia na Ubunifu kutoka Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof. Maulilio Kipanyula,akizungumzia Maonyesho ya Wiki ya Ubunifu 2023 inayowakutanisha wabunifu mbalimbali kutoka ndani na nje ya nchi yaliyoandaliwa na Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia yaliyoanza Aprili 24 hadi 28 mwaka huu  katika uwanja wa Jamhuri Jijini Dodoma.

Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Bi.Rosemary Senyamule,akigawa Vyeti pamoja na zawadi kwa washindi wa bunifu zao ambazo zimeshindanishwa na kukidhi viwango Vilivyotolewa na VETA wakati wa  Maonyesho ya Wiki ya Ubunifu 2023 inayowakutanisha wabunifu mbalimbali kutoka ndani na nje ya nchi yaliyoandaliwa na Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia yaliyoanza Aprili 24 hadi 28 mwaka huu  katika uwanja wa Jamhuri Jijini Dodoma.

Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Bi.Rosemary Senyamule,akiwa katika picha ya pamoja na washindi wa bunifu mbalimbali walioshinda wakati wa Maonyesho ya Wiki ya Ubunifu 2023 inayowakutanisha wabunifu mbalimbali kutoka ndani na nje ya nchi yaliyoandaliwa na Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia yaliyoanza Aprili 24 hadi 28 mwaka huu  katika uwanja wa Jamhuri Jijini Dodoma.

Na.Alex Sonna -DODOMA
Mkuu wa Mkoa wa Dodoma,Rosemary Senyamule amekoshwa na bunifu mbalimbali zilizopo katika maonesho ya wiki ya ubunifu  huku akiwaomba watanzania kufika katika uwanja wa Jamhuri kwa ajili ya kujionea.
Wiki ya ubunifu inawakutanisha wabunifu mbalimbali kutoka ndani na nje ya Nchi na ilianza  Aprili 24,2023 katika uwanja wa Jamhuri na  yanatarajia kumalizika Ijumaa Aprili 28 mwaka huu.
Akizungumza leo,Aprili 25,2023 mara baada ya kutembelea mabanda,Mkuu huyo wa Mkoa amesema   ameshuhudia mambo makubwa ambayo yamefanywa na wabunifu hao.
Ametoa shime kwa watanzania wengine kufika kwenye mabanda hayo kwa ajili ya kujionea bunifu hizo.
RC Senyamule amesema mambo mazuri aliyoyaona ni kijana mmoja kwenye banda la VETA ambaye ametengeneza miwani ambayo dereva akivaa kama akisinzia inamkumbusha kwa kupiga kengele kwa kumwambia asisinzie.
“Tunafahamu kwamba Serikali imekuwa ikihangaika muda mrefu jinsi gani ya kuzuia ajali sasa kijana wa kitanzania ametupatia ufumbuzi tunaimani teknolojia hiyo itaendelea kitumika kupunguza ajali nchini,”amesema Senyamule.
Amesema ubunifu huo ni wa kipekee kwani utasaidia sana hasa kwenye suala la usalama.
Aidha amesema pia amefurahishwa na banda la DIT ambao wametengeza gari linalotumia gesi.
“Na wamesema wameishaunganisha mfumo wa gesi kwenye magari mengi zaidi 2000 nimekuwa nikisikia leo nimejionea, inapunguza gharama za mafuta kwa zaidi ya asilimia 50,”amesema
Amesema kitu kingine kilichomfurahisha ni shule moja ya Arusha   wametengeneza gari la kutumia solar.
“Nimeona mabadiliko makubwa ya matumizi ya teknolojia na ubunifu mkubwa,nipongeze sana Wizara ya Elimu kwa kazi nzuri mnayofanya,”amesema RC Senyamule.
Aidha,RC Senyamule amesema maonesho hayo yamepiga hatua kwani ni halisi na kila mwaka yanaendelea kupiga hatua.
“Tumeweza kushuhudia baadhi ya bidhaa ambazo zinaweza kutumika katika maisha yetu ya kawaida  majumbani na maofisi.
“Kwa ujumla mimi nipongeze sana Serikali,nipongeze Wizara ya Elimu na taasisi zote ambazo zimeshiriki maonesho haya kwani yameendelea kuongeza thamani,”amesema RC Senyamule. 
Kwa upande wake Mkurugenzi wa Mafunzo ya Ufundi Stadi -VETA  Ndg.Abdallah Ngodu amesema kuwa maonesho ya wiki ya Ubunifu kwa mwaka huu yamekuwa tofauti sana kwani wamepewa nafasi ya kuwa na siku maalumu kwa ajili ya VETA ambayo imekwenda kwa jina la “VETA DAY”
Amesema  wameandaa vitu mbalimbali kutoka katika vyuo vya Veta.
Amesema wamekuwa na matukio muhimu ikiwemo mdahalo kwa ajili ya umuhimu wa elimu na Mafunzo ya Ufundi Stadi- katika ubunifu.
“Mdahalo huo utasimamiwa na Msemaji Mkuu wa Serikali ndugu Gerson Msigwa,”amesema.
Amesema wamekuwa na mashindano ya umahiri wa vijana ambao wanapata mafunzo katika vyuo vyao.
Ameeleza kuwa  vijana hao wameshindanishwa katika fani za ujenzi,Umeme na urembo.
Amesema wanalenga kujua vijana wamepata ujuzi na wameweza kumudu stadi zipi.
“Kutokana na tukio hili wamependekeza kwamba itakuwa endelevu na hao watakaoshinda watapata tuzo na vyeti,”amesema Ngodu.
Amesema mashindano hayo wamewashirikisha vijana waliohitimu au wale ambao ni wanufaika ambao wamekuja kuonesha kazi wanazofanya.
“Bahati nzuri katika hawa vijana waliomaliza vyuo vyetu wapo ambao wamaliza vyuo vikuu lakini kutokana na mazingira magumu ya ajira basi wamekuja VETA na wameweza kutengeneza vitu mbalimbali,”amesema Mkurugenzi huyo.
Aidha  ametoa wito kwa wananchi wafike katika uwanja wa Jamhuri kwa ajili ya kujionea kazi zinazofanywa na Veta.
“Sasa hivi tunatakribani vyuo 50 Nchi nzima ambavyo vinatoa mafunzo na Serikali imetoa fedha kwa ajili ya kujenga vyuo na kutakuwa na vyuo zaidi ya 140 maana yake kila Wilaya itakuwa na chuo,”amesema Mkurugenzi huyo.
Ngodu amemshukuru Rais Samia Suluhu Hassan kwa kuona umuhimu wa wananchi kupata stadi za ujuzi ili waweze kujiajiri.
Naye Mkurugenzi wa Idara ya Sayansi, Teknolojia na Ubunifu Prof.Maulilio Kipanyula amesema kuwa Maonesho ya wiki ya Ubunifu mwaka 2023 yamekuwa tofauti kwani imeanzi katika ngazi za mikoa na huko wabunifu walianza kuonesha bunifu zao katika ngazi hizo na sasa maonesho hayo yamefikia katika ngazi ya taifa hivyo imewapa nafasi wabunifu wengi kuonesha bunifu zao.
Prof. Kipanyula ameongeza kuwa katika maonesho hayo kutakuwa na siku maalumu kwa ajili ya Taasisi za VETA na Tume ya Nguvu za Atomiki Tanzania (TAEC) 
“VETA leo wameonesha bunifu zao na ndio maana leo ni VETA DAY dhumuni ni kuona ni namna gani uwekezaji uliofanywa na Serikali ya awamu ya sita katika elimu ya ufundi  imefanyiwa kazi na kuzalisha wabunifu wenye uwezo wa kuigiza sokoni bunifu kwa ajili ya kutatua changamoto za jamii,”
Na kuongeza kuwa “kwa upande wa Tume ya Nguvu za Atomiki Tanzania  (TAEC) nao watakuwa na TAEC DAY ambapo dhumuni la siku hiyo ni kuifanya Tume hiyo ijulikane na wananchi ,majukumu yake ni yapi, nini faida yake na mengine mengi ambayo yataelezwa.
Prof.Kipanyuka amewataka wananchi kujitokeza kwa wingi katika maonesho hayo ili kujionea bunifu mbalimbali ambayo zimebuniwa na wabunifu wa ndani huku ikichagizwa na wabunifu kutoka nchini Afrika Kusini  kwani lengo la serikali na Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia ni kuifanya wiki ya Ubunifu Tanzania kuwa ya kimataifa.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here