NA: FARIDA MANGUBE MOROGORO.
Naibu waziri wa ujenzi na uchukuzi Atupele Mwakibete ameitaka mamlaka ya hali ya hewa Tanzania (TMA) kusajili vituo vyote vya mamlaka hiyo kwa mujibu wa sheria ili kufikia malengo waliojiwekea kwa wakati na ubora unaotakiwa.
Aliyasema hayo wakati akifungua kikao cha baraza la kikao cha wajumbe na wafanyakazi TMA ambacho ni mahususi kwa kupitisha bajeti ya mwaka wa 2023na 2024 nakufanya tathini ya utendaji wa mamlaka hiyo.
Alisema Serikali ya awamu ya sita kwa kutambua umuhimu mkubwa wa kuboresha miundombinu ya huduma za hali ya hewa imefanya imefanya uimarishaji wa mtandao mkubwa wa rada na miundombinu nyingine ya hali ya weha na kuongeza uwezo wa nchi kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi.
Aidha ameitaka TMA kuongeza ubunifu katika kuongeza vyanzo vya ukusanyaji wa mapato na kusimamia vyanzo hivyo mapato ili kupunguza utegemezi kutoka serikalini.
Awali akizungumza katika ufunguzi huo Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa TMA Dkt.Ladsilaus Chang’a alisema kuwa kikao hicho ni uthibitiisho wa ushirikiano mkubwa na ushilikishwaji wa wafanyakazi katika maendeleo ya taasisi pamoja na nakushughulikia maswala mtambuka ikiwemo maslahi ya wafanyakazi.
“Madhumuhi makubwa ya baraza hili ni kupokea kujadili na kupitisha mapendekezo ya bajeti ya mamlaka ya kipindi cha mwaka wa fedha 2023na 2024 mapendekezo hayo ya bajeti yanazingatia vipaumbele yanayowezesha mamlaka kufikia malengo yake kuongeza ubora na ufanisi katika utoaji wa huduma kwa umma.” Alisema Dkt. Chang’a.
Kwa upandea wake Meneja wa utawala na lasirimali watu TMA Mariam IS-haaq amesma kuwa ni fursa kwa baraza hilo kupata elimu ili kuboresha shughuli zinazofanyika na kupanga mipango na mikakati mbalimbali.