Home BUSINESS SUA YAZINDUA KAMATI YA USHAURI WA VIWANDA CHINI YA MRADI WA HEET

SUA YAZINDUA KAMATI YA USHAURI WA VIWANDA CHINI YA MRADI WA HEET

Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia anayeshughulikia Elimu ya Juu Prof . James Mdoe akikata utepe kuashiria kuzinduzi  wa Kamati ya Ushauri wa Viwanda iliyo chini ya mradi wa HEET,  tarehe 28.4 . 2023 Mjini Morogoro.

Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia anayeshughulikia Elimu ya Juu Prof . James Mdoe akiwa katika picha ya Pamoja  mara baada ya  kuzindua  Kamati ya Ushauri wa Viwanda iliyo chini ya mradi wa HEET, tarehe 28.4 . 2023 Mjini Morogoro.

NA: FARIDA MANGUBE, MOROGORO.

Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia anayeshughulikia Elimu ya Juu Prof . James Mdoe amesema utekelezaji wa Mradi wa Elimu ya Juu kwa Mageuzi ya Kiuchumi yaani (Higher Education for Economic Transformation [HEET] project) unaofadhiliwa na Benki ya Dunia, unalenga  Kukuza na kuinua uchumi nchini kupitia Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia ambapo  Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo (SUA) ni miongoni mwa wanufaika mradi huo.

Prof. Mdoe ameyasema hayo wakati wa kuzindua Kamati ya Ushauri wa Viwanda iliyo chini ya mradi wa HEET kwa niaba ya Waziri wa Elimu Sayansi na Teknolojia Prof. Adolf Mkenda amesema kuwa zoezi hilo ni moja ya utekelezaji Ilani ya Chama cha Mapinduzi (CCM) 2020 -2025 kuufikisha mradi huo kukamilika kwa ubora na wakati ili kuboresha Elimu ya Juu

Aidha amesema kuwa hapo awali hapakuwa na mfumo rasmi kwa Vyuo Vikuu kuwezesha kukaa pamoja na kuchakata mahitaji muhimu ili kufanikisha Elimu Bora pia ajira imepelekea kuwa na ombwe na sasa imekuwa rasmi Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo kama moja ya wanufaika na mradi wa HEET kamati hiyo ikasaidie kutoa wanafunzi wenye taaluma na wanaohitajika katika ulimwengu wa kazi na kufikia malengo ya viongozi wao nchini.

Naye Mwakilishi kutoka Benki ya Dunia Bw. Kaboko Mkalinga amewataka waajiri kujitoa vyema katika utekelezaji wa mradi huo kutokana na uzoefu walionao hivyo wahakikishe wanatoa mchango wao kwa wananchi na kuhakikisha mradi huo unafanikiwa kwa kutengeneza uzalishaji wa ajira nchini.

Kwa upande wake Mwakilishi wa Mkurugenzi Mtendaji wa  Shirikisho la Viwanda nchini Tanzania Bw. Akida Mnyenyelwa amesema kamati iliyochaguliwa ni muhimu kwa lengo la kuleta maendeleo ya viwanda hivyo kamati hiyo iliyoundwa ikatekeleze majukumu yake ikizingatia sekta hiyo na umuhimu wa viwanda nchini.

Aidha Bw. Mnyenyelwa amevitaka Vyuo kuwa na ushirikiano na wenye viwanda na kujua viwanda vinavyoendeshwa ili iwasaidie kutengeneza mitaala yenye kuleta tija kwa kutambua fani na ujuzi unaohitajika kwenye viwanda pia tafiti zitakazofanywa zinazohusu viwanda kutoka SUA na Vyuo vingine nchini wahakikishe wanaleta mrejesho kwa wamiliki wa viwanda ili kutambua changamoto na wapi pa kufanyia kazi.

Akizungumzia majukumu ya wajumbe wa kamati iliyozinduliwa Dkt. Felix Nandonde, Kiongozi wa mradi wa HEET upande wa Uhusiano na Taasisi Binafsi kutoka SUA amesema kuna majukumu 11 katika utekelezaji wa mradi huo lakini ameyataja majukumu manne ambayo yanawalenga moja kwa moja ikiwa ni pamoja na kubuni na kutekeleza mipango bora katika kutengeneza ajira, kushauri Chuo katika kubuni mitaala bora yenye uhitaji,kutafuta nafasi za mafunzo kwa vitendo ya muda mrefu kwa wanafunzi na Wahadhiri,kushawishi sekta binafsi kuweka fedha katika tafiti za Chuo

Awali kabla ya kumkaribisa mgeni rasmi Mratibu wa Mradi wa Elimu ya Juu kwa Mageuzi ya Kiuchumi (HEET) Prof. Amandus Muhairwa amesema kuwa SUA imepokea kiasi cha shilingi Milioni 73.6 ambazo ni sawa na Dola za kimarekani Millioni 32 ambazo zimegawanywa kutumika katika makundi mawili ambayo Milioni 55.2 zitatumika Kampasi Kuu ya Edward Moringe na kiasi cha shilingi milioni 18.4 kitatumika Kampasi yao ya Katavi kwa lengo la kuboresha elimu kwa Chuo hicho

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here