Home SPORTS SIMBA SC YAPOKEA KICHAPO CHA 3-1 NA RAJA CASABLANCA

SIMBA SC YAPOKEA KICHAPO CHA 3-1 NA RAJA CASABLANCA

KLABU ya wekundu wa msimbazi Simba SC imepoteza mchezo wake wa marudiano kwa kukubali kichapo cha magoli 3-1 dhidi ya Raja Casablanca ya Morocco mchezo uliochezwa nchini usiku wa kuamkia leo April 1, 2023 nchini humo.

Katika kipindi cha kwanza cha mchezo huo timu ya Simba ilicheza kwa umakini mkubwa na kufanikiwa kwenda mapumziko bila kuruhusu  goli.

Kipindi cha pili kilianza kwa kasi kubwa huku Kila timu ikilisakama lango la mwenzake ambapo Raja Casablanca ndio ilikuwa ya kwanza kuzifumania nyavu za mnyama huyo huku timu ya Simba ikisawazisha ndani ya dakika chache baadae goli likifungwa na Jian Baleke.

Hata hivyo Raja Casablanca walipata mkwaju wa Penati dakika ya 70 na kufanikiwa kupata goli la pili, na baadaye kuongeza la tatu.

Simba sasa inarejea nyumbani kusubiri ratiba ya CAF kuelekea hatua ya robo fainali.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here