Home SPORTS SIMBA SC YAIDUWAZA YANGA, IKIICHAPA 2-0 KWA MKAPA

SIMBA SC YAIDUWAZA YANGA, IKIICHAPA 2-0 KWA MKAPA

KLABU ya wekundu wa msimbazi Simba SC imewaadhibu watani wao wa jadi Yanga SC  mabao 2-0 katika mchezo wa Ligi Kuu ya NBC mchezo uliopigwa katika Dimba la Mkapa Jijini Dar es Salaam.

Magoli ya Simba yalipachikwa kambani na Frank Inonga akipiga kichwa kuunganisha mpira wa kona katika dakika za mwanzoni za kipindi cha kwanza katika mchezo huo.

Goli la pili liliwekwa kambani na Kibu Denis katika dakika ya 31 ya Kipindi cha kwanza cha mchezo huo kwa shuti Kali lililomshinda mlinda mlango wa Wananchi Didie.Diara goli liliodumu hadi kipindi cha kwanza kinamalizika.

Kipindi cha pili kilianza kwa kasi huku kila timu ikifanya mabadiliko na kucheza kwa kasi ikilisakama lango la mwenzake. 

Kufuatia mchezo huo timu ya Simba SC inabaki katika nafasi ya pili ya Ligi ya NBC ikiwa na alama 63 huku wapinzani wao Yanga SC ikibaki kileleni mwa msimamo wa ligi hiyo wakiwa na alama 65 wakiwa na tofauti ya alama 2.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here