Home BUSINESS SERIKALI YATOA UFAFANUZI WA MALALAMIKO YA SARUJI YA HAUXIN

SERIKALI YATOA UFAFANUZI WA MALALAMIKO YA SARUJI YA HAUXIN

Naibu Waziri wa Uwekezaji, Viwanda na Biashara Mhe. Exaud Kigahe (Mb), akizungumza alipokuwa akitoa ufafanuzi kuhusu malalamiko ya Saruji aina ya Hauxin inayozalishwa na Kiwanda cha Maweni Limestone Limited kilichopo Tanga, pamoja na kueleza mwendendo wa bei za bidhaa muhimu nchini kwa Mwezi Machi na Aprili 2023 katika mkutano na waandishi wa habari uliofanyika April 13 Jijini Dodoma.

Sehemu ya waandishi wa Habari walioshiriki mkutano huo wakifuatilia maelezo ya Naibu waziri Kigahe.

Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini, Wizara ya Uwekezaji, Viwanda na Biashara Bi Suzan Mshakangoto akizungumza alipokuwa akiwakaribisha waandishi wa habari (hawapo pichani) katika mkutano huo.

(PICHA NA WZUVB)

DODOMA.

Naibu Waziri wa Uwekezaji, Viwanda na Biashara Mhe. Exaud Kigahe (Mb.) ametoa rai kwa wazalishaji wa bidhaa zote za viwandani kuongeza jitihada za uzalishaji wa bidhaa kwa ubora unaohitajika sokoni na kwa kufuata Sheria, Kanuni na Taratibu zilizowekwa ili kukabiliana na mfumuko wa bei za bidhaa mbalimbali.

Ameyasema hayo April 13, 2023 alipokuwa akifafanua zaidi kuhusu malalamiko ya Saruji aina ya Hauxin inayozalishwa na Kiwanda cha Maweni Limestone Limited kilichopo Tanga kuhusu upungufu wa uzito wa bidhaa hiyo wakati akizungumza na waandishi wa habari kuhusu mwenendo wa bei za mazao ya chakula na bidhaa muhimu nchini kwa mwezi Machi hadi Aprili 2023

Kigahe amesema kwa mujibu wa wa kifungu namba 41(a) na (b) cha Sheria ya Vipimo ya 2016 Sura ya 340, kinatoa katazo kwa mtu yeyote kuuza bidhaa yoyote iliyo chini ya uzito, kipimo au namba.

Aidha amesema Sheria hiyo inatoa katazo kwa mtu yeyote katika ufanyaji biashara kutoa taarifa za uongo juu ya bidhaa yoyote kuhusu uzito, kipimo, namba, geji au kiwango. Endapo makosa haya yatafanyika mtu huyo ametenda kosa kwa mujibu wa Sheria hii.

Dkt. Kigahe pia amesema Sheria hiyo imempa mamlaka Kamishna wa Wakala wa Vipimo kufifisha kosa (compounding of offences) na kumtoza faini mtu huyu ya kiasi kwa mujibu wa kifungu cha 46 cha Sheria ya Vipimo kama kilivyofanyiwa marekebisho na kifungu cha 48 cha Sheria ya marekebisho mbalimbali ya Sheria Na. 3 ya mwaka 2016.

Kwa upande wa mwendendo wa bei za bidhaa muhimu nchini kwa Mwezi Machi na Aprili 2023, Mhe. Kigahe amesema wastani bei za mazao yote na bidhaa za chakula ikiwemo mchele,mahindi,unga wa mahindi,maharage zimeshuka kwa asilimia kati 0.8 na 7.0 huku bei ya vifaa vya ujenzi imeendelea kuwa himilivu kwa kutokuwa na mabadiliko.

Vilevile amewahakikishia wananchi kuwa Serikali  inaendelea kuchukua hatua mbalimbali katika kudhibiti ongezeko la bei za bidhaa muhimu nchini hasa katika kipindi hiki cha Mfungo Mtukufu wa Ramadhan.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here