Home LOCAL MSD YANUNUA MASHINE 140 KWA AJILI YA KUSAFISHA DAMU KWA WAGONJWA WA...

MSD YANUNUA MASHINE 140 KWA AJILI YA KUSAFISHA DAMU KWA WAGONJWA WA FIGO

Mfamasia Mkuu wa Serikali Daudi Msasi akizungumza kwa niaba ya katibu Mkuu wa Wizara ya Afya katika Semina ya siku mbili ya Wahariri wa vyombo vya Habari iliyoandaliwa na Bohari ya Dawa-(MSD) Mkoani Dodoma.

Mkurugenzi Mkuu wa Bohari ya Dawa-MSD Mavere Tukai akizungumza alipokuwa akitoa hotuba yake katika semina hiyo inaofanyika kwa siku mbili April 5 na 6, 2023 Mkoani Dodoma.

Msemaji Mkuu wa Serikali na Mkurugenzi wa Idara ya Habari Maelezo Gerson Msigwa akizungumza na Wahariri wa Vyombo vya habari, pamoja na watumishi mbalimbali wa MSD (hawamo pichani) katika mkutano huo.

Meneja Mawasiliano na Uhusiano wa MSD Etty Kusiluka akizungumza alipokua akiwakaribisha Wahariri na kutoa utambulisho kwa viongozi waliofika katika Semina hiyo.

(PICHA NA: HUGHES DUGILO)

Na: Hughes Dugilo, DODOMA.

Serikali kupitia Bohari ya Dawa(MSD) tayari imeshanunua mashine 140 kwa ajili ya kusafisha damu kwa wagonjwa wa figo na kwamba tayari zimeshasambazwa kwenye hospitali 14 na kati hizo hospitali tano mashine zimeshafungwa na kuanza kufanya kazi.

Hayo yamebainishwa na Mfamasia Mkuu wa Serikali Daudi Msasi alipokuwa akifungua Semina ya Wahariri wa Vyombo vya habari kwa niaba ya Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya Dkt. Seif Shekalaghe inayofanyika kwa siku mbili April 5 Hadi 6, 2023 Jijini Dodoma.

Amezitaja Hospitali zilizowekwa mashine hizo ni Chuo Kikuu Cha Dodoma (UDOM) Hospitali ya Rufaa Amana, Hospitali ya Rufaa ya Kanda Chato, Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Pwani Tumbi, Hospitali ya Rufaa ya Mkoa SekouToure.

“Rais wetu Dkt Samia Suluhu Hassan katika kipindi chake cha miaka miwili ameipa kipaumbele MSD na kusababisha isambaze Dawa kwa wakati na ubora” amesema Msasi.

Kwa upande Mkurugenzi wa Uendeshaji wa MSD Billy Singano, amesema kuwa uamuzi wa MSD kuamua kununua mashine hizo 140 kutasaidia kupunguza gharama za kusafisha damu kwa wagonjwa wa figo nchini.

“Hapo awali wananchi walikuwa wanakwenda nje ya nchi kutafuta huduma hiyo ya kuchuja damu kwa wagonjwa wa Figo lakini sasa Serikali yetu imewezesha huduma hizi kupatikana hapa nchini” amesema Singano.

Kwa mujibu wa MSD mashine hizo zote zitakapofungwa zitasaidia kuwapunguzia gharama wananchi na ikumbukwe kuwa mashine hizo hapo awali zilikuwa zinanunuliwa na watu binafsi.

Awali Akizungumza katika Semina hiyo Mkurugenzi Mkuu wa MSD Mavere Tukai amesema kuwa Taasisi hiyo inafanyakazi kwa kuzingatia ubora unaostahili ili kulinda afya za wananchi.

Aidha amesema lengo la kuandaa Semina hiyo kwa Wahariri wa Vyombo vya habari ni kutoa ufafanuzi juu ya masuala mbalimbali yanayojitokeza katika jamii ili kufahamu namna taasisi hiyo inavyotekeleza majukumu yake.

Mkurugenzi wa Uendeshaji wa Mamlaka ya Dawa na Vifaa Tiba (TMDA) akizungumza kwa niaba ya Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi hiyo Adam Fimbo.

Meneja Masoko wa NHIF Hipolitti akitoa salamu zake kwa niaba ya Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi hiyo.

Mwenyekiti wa Jukwaa la Wahariri Tanzania (TEF) katika Semina hiyo.

 

Previous articleYASEMAVYO MAGAZETI YA LEO JUMATANO APRILI 5,2023
Next articleHAKUNA WILAYA ITAYOKOSA GARI LA KUBEBEA WAGONJWA, MAGARI 727 YANUNULIWA.
Hughes Dugilo is a Writer, News Producer, Video-Photographer Journalist, and Video Editor experienced for 20 years now performing in News, Documentary, Advertisements and Television Programs. Aside from all above he own and operate his Blog known as Green Waves Media TZ since 2018.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here