Home LOCAL RAIS SAMIA AKUTANA NA MTOTO HAMIMU MWENYE MATATIZO YA NGOZI, IKULU JIJINI...

RAIS SAMIA AKUTANA NA MTOTO HAMIMU MWENYE MATATIZO YA NGOZI, IKULU JIJINI DAR ES SALAAM

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akimsikiliza Mtoto Hamimu Mustapha Baranyikwa (15) mwenye matatizo ya ngozi ambaye ni mkazi wa Nyakanazi Mkoani Kagera. Mtoto huyo Hamimu alifika Ikulu kwa ajili ya kumshukuru Mhe. Rais kwa msaada wa matibabu aliompatia katika Hospitali ya Taifa Muhimbili Jijini Dar es Salaam. Rais alimuona mtoto huyo kwa mara ya kwanza wakati wa Ziara yake Nyakanazi Mkoani Kagera tarehe 16 Oktoba, 2022 na kuagiza apatiwe matibabu baada ya kuhangaika kwa muda mrefu.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa kwenye mazungumzo na mtoto Hamimu Mustapha Baranyikwa (15) mwenye matatizo ya ngozi ambaye alikuwa na shauku kubwa ya kumuona Mhe. Rais Samia. Pichani mtoto huyo akiwa haamini macho yake mara baada ya kugundua kuwa aliyekuwa anazungumza naye ni Mhe. Rais Samia, Ikulu Jijini Dar es Salaam.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa kwenye picha ya pamoja na mtoto Hamimu Mustapha Baranyikwa (15) mwenye matatizo ya ngozi ambaye alifika Ikulu Jijini Dar es Salaam kwa ajili ya kumshukuru kwa msaada aliompatia wa matibabu katika Hospitali ya Taifa Muhimbili.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akimkaribisha Mtoto Hamimu Mustapha Baranyikwa (15) mwenye matatizo ya ngozi, Ikulu Jijini Dar es Salaam. Wa kwanza kulia ni Kaka wa mtoto huyo Saddam Mustapha Baranyikwa.

Previous articleSERIKALI IMETENGA BIL. 9.9 UJENZI WA VITUO SABA VYA ZIMAMOTO NA UOKOAJI-MAJALIWA
Next articleWATU WALIOGOPA KUMSOGELEA; RAIS SAMIA AKAMSHIKA MKONO NA KUOKOA MAISHA YAKE
Hughes Dugilo is a Writer, News Producer, Video-Photographer Journalist, and Video Editor experienced for 20 years now performing in News, Documentary, Advertisements and Television Programs. Aside from all above he own and operate his Blog known as Green Waves Media TZ since 2018.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here