Home LOCAL RAIS SAMIA AFANYA MABADILIKO BARAZA LA MAWAZIRI

RAIS SAMIA AFANYA MABADILIKO BARAZA LA MAWAZIRI

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan amefanya mabadiliko madogo ya Baraza la Mawaziri kama ifuatavyo:
  1. Amemteua Mhe. Jenista Joakim Mhagama (Mb) kuwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu). Mhe. Mhagama anachukua nafasi ya Mhe. George Boniface Simbachawene (Mb). Kabla ya uteuzi huo alikuwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora.
  1. Amemteua Bw. George Boniface Simbachawene (Mb) kuwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora. Mhe. Simbachawene anachukua nafasi ya Mhe. Jenista J. Mhagama (Mb). Kabla ya uteuzi huo Mhe. Simbachawene alikuwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu).

Uteuzi huu umeanza tarehe 01 Aprili, 2023.

Mawaziri wateule wataapishwa tarehe 02 Aprili, 2023 saa 3 asubuhi, Ikulu,    Dar es Salaam.

Zuhura Yunus
Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, Ikulu

Previous articleWAZIRI MKUU AWAAGIZA WAKUU WA MIKOA 12 WASIMAMIE LISHE BORA
Next articleBENKI KUU YA TANZANIA YATOA ELIMU CHUO CHA SAYANSI NA TEKNOLOJIA MBEYA (MUST)
Hughes Dugilo is a Writer, News Producer, Video-Photographer Journalist, and Video Editor experienced for 20 years now performing in News, Documentary, Advertisements and Television Programs. Aside from all above he own and operate his Blog known as Green Waves Media TZ since 2018.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here