Home ENTERTAINMENTS RAIS MSTAAFU KIKWETE AMTAKIA AFYA NJEMA MSAMA

RAIS MSTAAFU KIKWETE AMTAKIA AFYA NJEMA MSAMA

Rais Mstaafu wa Awamu ya Nne Mhe. Dkt Jakaya Mrisho kikwete amemtakia afya njema mfanyabiashara maarufu ambaye ni Mkurugenzi wa Msama Promotions na Dira media group Alex Msama baada ya siku chache kuugua ghafla na kulazwa katika Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI) Jijini Dar es Salaam kabla ya kuhamishiwa Moi anapopatiwa matibabu zaidi kwa sasa.

Kwa mujibu wa watu wa karibu wa Alex Msama Rais Kikwete amemtakia afya njema ili aweze kupona Mkurugenzi huyo tayari kwa ajili ya kuendelea na shughuli zake za kujenga nchi, ambazo amekuwa akizifanya.

Msama kwasasa anaendelea na matibabu katika hospital ya moi Jijini Dar es Salaam.

Previous articleYASEMAVYO MAGAZETI YA LEO JUMATATU APRILI 24,2023
Next articleHUDUMA ZA UCHUNGUZI NA UPASUAJI ZAIMARISHWA NAMTUMBO
Hughes Dugilo is a Writer, News Producer, Video-Photographer Journalist, and Video Editor experienced for 20 years now performing in News, Documentary, Advertisements and Television Programs. Aside from all above he own and operate his Blog known as Green Waves Media TZ since 2018.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here