Home LOCAL RAIS DKT. SAMIA AWAAPISHA MAWAZIRI JENISTA MHAGAMA NA SIMBACHAWENE IKULU DAR ES...

RAIS DKT. SAMIA AWAAPISHA MAWAZIRI JENISTA MHAGAMA NA SIMBACHAWENE IKULU DAR ES SALAAM LEO

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akimuapisha Mhe. Jenista Mhagama kuwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu) kwenye hafla fupi iliyofanyika Ikulu Jijini Dar es Salaam tarehe 02 Aprili, 2023.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akimuapisha Mhe. George Simbachawene kuwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais (Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora) tarehe 02 Aprili, 2023.

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu) Mhe. Jenista Mhagama, pamoja na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais (Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora) Mhe. George Simbachawene wakila Kiapo cha Uadilifu kwa Viongozi, Ikulu Jijini Dar es Salaam tarehe 02 Aprili, 2023.

Viongozi mbalimbali waliohudhuria hafla ya Uapisho wa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu) Mhe. Jenista Mhagama, pamoja na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais (Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora) Mhe. George Simbachawene, Ikulu Jijini Dar es Salaam tarehe 02 Aprili, 2023.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here