Home LOCAL MVOMERO YAJA NA MKAKATI WA KUDHIBITI MIGOGORO YA ARDHI.

MVOMERO YAJA NA MKAKATI WA KUDHIBITI MIGOGORO YA ARDHI.

NA: FARIDA MANGUBE, MOROGORO.

Uongozi wa Wilaya Mvomero Mkoani Morogoro umeandaa mpango maalumu kukabiliana na migogoro ya ardhi hasa ya wakulima na wafugaji ambayo imekuwa tatizo sugu ndani ya wilaya hiyo kwa kuanza kuwachukulia hatua za kisheria wanaochochea migogoro hiyo ikiwemo wanaopokea wageni wanaoingia kinyemela.

Mwenyekiti wa kamati ya usalama na Mkuu wa wilaya hiyo ya Mvomero Judith Nguli amesema kuwa kamati ya usalama wamefanya vikao mbalimbali vilivyowashirikisha viongozi wa viijiji, wafugaji pamoja na wakulima ambapo tayari wamepata majina ya wanaodaiwa kuwa wachochezi.

“Tuliwaeleza wafugaji wote ndani ya Wilaya ya Mvomero kama haupo sehemu ambayo haijatengwa kwa ajili ya eneo la ufugaji basi unatakiwa kufungia mifugo yako kwa kujenga uzio ili kuzuia mifugo hiyo kuingia kwenye mashamba ya wakulima”. alisema Nguli

Amewataka wakulima wanaolishiwa mazao yao pamoja na kesi ya jinai pia wafungue kesi ya madai ambayo itampa fursa mkulima kulipwa fidia yake bila kupata changamoto yoyote pamoja na kutoa ushirikiano kwa mahakama.

Akizungumza Kwenye baraza hilo Diwani wa kata ya Mangae Leila Jakwanga ameishukuru kamati hiyo kwani migogoro ya wakulima na wafugaji ilikuwa tishio ndani ya wilaya hiyo.

Mwenyekiti wa baraza la madiwani ya Halmashauri hiyo Yusuph Makunjaasema migogoro inachelewasha masuala ya maendeleo katika maneo yao vhivyo mpango ulipo kwa sasa ni kusimamia sheria ndogo walizojiwekea pamoja na kuwafikisha kwenye vyombo vya kisheria wale wanaobanika kuwa chanzo cha migogoro.

MWISHO.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here