Home LOCAL MSD KANDA YA KATI, WADAU WAKUTANA KUJADILI KUBORESHA HUDUMA ZA AFYA

MSD KANDA YA KATI, WADAU WAKUTANA KUJADILI KUBORESHA HUDUMA ZA AFYA

Na: MWANDISHI WETU

BOHARI ya Dawa (MSD) Kanda ya Kati Dodoma imekutana na wadau na wateja wake wakiwemo waganga wakuu, wafamasia na watendaji wa halamshauri kuhakikisha wanajadili uboreshaji wa huduma za afya na upatikanaji wa dawa na vifaa tiba kwa uhakika kupunguza kero kwa wananchi.

Katika mkutano huo wadau hao wamekubaliana kuunga mkono jitihada za Rais Dk.Samia Suluhu Hassan za maboresho sekta ya afya kwa vitendo kwa kutumia taaluma zao kutoa huduma stahiki.

Akizungumza jana wilayani Kondoa mkoani Dodoma Meneja wa MSD Kanda ya Kati John Sipendi alisema, lengo la bohari kurejesha mikutajo hiyo ya pamoja na wadau ni kukubali kukoselewa, kujenga mazingira ya kupunguza changamoto za pande zote mbili, kubadilisha uzoefu na kukubaliana kufanya kazi kwa pamoja bila kutafuta mshindi kwa kuwa wote wanamuhudumia mwananchi wa Tanzania.

Alisema, kikao kazi hicho kati ya watendaji wa MSD wa Kanda na Makao Makuu, wadau na wateja wake wakiwemo waganga wakuu wafamasia na watendaji wa halamshauri ni kuhakikisha wanajadili uboreshaji wa huduma za afya na upatikanaji wa dawa na vifaa tiba kwa uhakika kupunguza kero kwa jamii.

“Kwa kutambua umuhimu wa ushirikiano kati yetu na wadau wa afya mkutano huu umeazimia kuunga mkono jitihada za Rais Dk.Samia za amboresho sekta ya afya kwa vitendo kwa kutumia taaluma zetu kutoa huduma stahiki na kwa wakati,”alisema.

Kwa upande wake Katibu Tawala wa Mkoa wa Dodoma, Ally Gugu, alisema katika kikao hicho kikichoshirikisha watendaji wenye ngazi ya maamuzi wa mkoa wa Dodoma na maeneo ya jirani ikiwemo Singida na Manyara kwa pamoja wamejadili maboresho ya ufikashaji wa dawa na vifaa tiba katika vituo vya kutolea huduma na namna ya kushirikiana katika kumpatia mtanzania huduma bora za afya.

Alisema, wamebaini zipo changamoto zinazoweza kutatuliwa kwa pamoja ikiwemo eneo la maoteo, bajeti za vituo na mahitaji ya bidhaa hizo kulingana na wakati uliopo ili kupunguza uharibu wa dawa zinazoteketezwa na kuiingizia serikali hasara.

Naye Mganga Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Dk. Best Magoma, alisena watahakikisha kazi kubwa iliyofanywa na Rais Dk. Samia inaonekana kwa kutimiza wajibu wao kwa walengwa ambao ni wananchi kufikiwa na huduma bora za afya.

Ivon Mwingie ambaye ni Mfamasia Mkuu wa Hospitali ya Taifa ya Afya ya Akili ya Milembe iliyopo Dodoma, alisema kikao kazi hicho ni muhimu na kina afya kwa watendaji katika kuboresha upatikanaji wa huduma kwa wananchi, kuliko mihimili ya serikali yenye jukumu moja kubaki kunyoosheana vidole.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here