Home SPORTS MGANGA MKUU DSM MGENI RASMI BONANZA LA UCHANGIAJI DAMU SALAMA

MGANGA MKUU DSM MGENI RASMI BONANZA LA UCHANGIAJI DAMU SALAMA

Mganga mkuu wa mkoa wa Dar es salam Dkt Rashid Mfaume atakuwa mgeni Rasmi katika Bonanza la uchangiaji damu salama litakalo fanyika tarehe 6 Mei wazo mivumoni.

Hayo yamesemwa na muandaaji wa Bonanza hilo Anjela Seth ambaye pia ni mwandishi kutoka fullshangweblog alipokuwa akiongea na wanahabari leo katika ufunguzi wa Ligi ndogo ya hamasa itakayochezwa kwa wiki mbili eneo la wazo huku timu kumi zikishiriki.

Aidha Anjela amesema nia na madhumuni ya ligi hiyo kuchezeshwa ni kutoa elimu na hamasa kwa wananchi juu ya uchangiaji damu salama kwa hiyari.

Kwa upande wake Mchungaji Richard Hananja ambaye ni mlezi wa Bonanza la uchangiaji damu salama Amesema anamshukuru Anjela kwa kuhamasisha uchangiaji wa damu salama kwani ni jambo jema na yeye yupo tayari kuendelea kuhamasisha viongozi wa Dini waweze kuhamasisha waumini wao kushiriki zoezi la uchangiaji damu salama kwa hiyari siku husika.

Naye Fatuma R. Mjungu ambaye ni Afisa Uhamasishaji kutoka Mpango wa Taifa Damu salama kanda ya mashariki amewahamasisha wananchi wa kata ya wazo, Wilaya kinondoni na mkoa kwa ujumla kushiriki zoezi la uchangiaji damu salama kwa hiyari siku husika.

Previous articleMRADI WA AFYA YA MACHO WA Sightsavers WATOA MATUMAINI KWA MAMILIONI YA WATU KUEPUKA JANGA LA KITAIFA LA UONI
Next articleMBETO: ASEMA CCM INAJIIMARISHA KISIASA NA KIJAMII
Hughes Dugilo is a Writer, News Producer, Video-Photographer Journalist, and Video Editor experienced for 20 years now performing in News, Documentary, Advertisements and Television Programs. Aside from all above he own and operate his Blog known as Green Waves Media TZ since 2018.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here