Home LOCAL MAHAKAMA YAWANOA WAHARIRI NA WAANDISHI WA HABARI ZA MAHAKAMANI

MAHAKAMA YAWANOA WAHARIRI NA WAANDISHI WA HABARI ZA MAHAKAMANI

Na: Farida Mangube Morogoro.
MAHAKAMA ya Tanzania imetoa wito kwa wadau wegine wa mahakama hiyo kutumia mifumo ya Tehema ili kurahisha usikilizwaji wa  mashauri ili kuendana na kasi ya muhimili huo uliojitanabaisha kwenye matumizi ya Teknolojia .
Hayo yametanabaishwa leo tarehe 3 Aprili 2023 kwenye mafunzo kwa waandishi wa habari za mahakamani,wahariri na maafisa habari yanayofanyika mkoani Morogoro yenye lengo la kuwapa uelewa wanahabari juu ya  mwenendo mahakama  kwenye matumizi ya Teknolojia.
Akizungumza wakati wa uzinduzi wa mafunzo  hayo Jaji Mfawidhi Mahakama kuu kanda ya  Morogoro Paul Ngwembe, amesema kuwa mahakama imepiga hatua kubwa kwenye matumizi ya Tehama kwa kumiliki mifumo mbalimbali inayowezesha kazi zake kirahisi hivyo ametoa wito kwa wadau wengine kuendana na mwendo huo.
“Nitoe wito kwa wenzetu ,Ofisi ya Mwendesha Mashtaka (DPP), Mawakili wa Serikali, na Mawakili wa kujitegemea kuiga mfano wa Mahakama katika masuala ya Teknolojia ili kusudia twende pamoja mahakama haiwezi kutekeleza majukumu yake ikiwa wenzetu wadau muhimu wakiwa nyuma tunataka na wananvchi waijue vizuri mifumo hii ili waweze kuendesha mashaufi yao bila gharama kubwa” amesema Jaji Ngwembe.
“Mifumo hiyo ni pamoja Mfumo  wa Tanzili ambao huchapisha  uamuzi, sheria na kanuni umefanya vizuri na kuifanya mahakama ya Tanzania kuwa ya kwanza Duniani  kutembelewa na watu wangi kwa asilimia 82.7 ambapo nchi inayoifuta tanzania yenye mfumo kama huo ana asilimi 2.4 hapo unaona kwa namna ambavyo tulivyokuwa kinara” Jaji Ngwembe.
Amesema kuwa mfumo huo unaonyesha hukumu kwa uwazi pale ambapo inapotolewa pia unaonyensha mashauri takribani 32 yanayoendelea duniani na kwamba ni mfumo rahisi kutumia nan hauna gharama kubwa .
Jaji Ngwembe amesema kuwa Mfumo mwengine ni JSDS 2)  mfumo wa  kieletroni wa kusajili mashauri na kesi mbalimbali bila kufika mahakamani na kusikilizwa.
“Tangu tumekuwa na mfumo huu tumerahisisha usikilizwaji wa mashauri huhitaji kufika mahakamani unaweza kufungua shauri kwa njia ya tehama na shauri likasikilizwa mfumo huu unakwenda sambamba na mfumo usikizwaji wa kesi kwa njia ya video (Video Confrence)”amesema Jaji Ngwembe.
Jaji Ngwembe amesema Mfumo wa tatau unawasajili na  kuwatambua mawakili wa mahakama “umeleta matunda makubwa kwa mahakama kwa kuwezesha kutekeleza majukumu yake na kuwafichua mawakili vishoka ambapo walikuwa wanajifanya wanasheria, mahakimu au mawakili bila kuwa na sifa zinazowezesha kuwa mawakili, hivyo mfumo huo umepunguza kwa kwa kiasi kikubwa  uhalifu wa kisheria”
Amesema kuwa sheria hamruhusu mtu asiye na sifa za kuwa wakili kufanya kazi ya uwakili na kwamba mwananchi kupitia mfumo huo atamtambua mtu mwenye sifa ya kufanya kazi ya uwakili kwa kuwa mfumo huo unaweka picha na jina la wakili anayestahili kufanya kazi.
Amesema kuwa mfumo wa nne unaowezesha mahakama kufanya kazi zake ni ule mfumo wa kusikiliza mashauri kwa njia ya video yaani Video Conference ambapo mfumo huo unanganisha Magereza, mahakama, wakili, Ofisi ya DDP .
“Mfumo huu unaweza kusiliza shauri bila kufika mahakamani mimi nimesikiliza mashauli na mashahidi  kutoka Kigoma , Mtwara, au Sumbawanga nikiwa hapa Morogoro  shahidi anatoa ushahidi wake mpaka anamaliza na tunamuuliza maswali mpaka tunamaliza, mfumo huu wananchi wakiuelewa  vizuri kutasaidia kupunga gharama za kuendesha mashauri “ amesema Jaji Ngwembe.
Amesema kuwa Mahakama haijishia hapo imeongeza ufanisi wa utoaji elimu ya sheria kwa wananchi kwa kuanzisha kituo cha kupokea simu za wananchi ili kuwafahamisha masuala mbalimbali ya kisheria “wananchi wanapiga simu moja kwa moja na hupokelwa kwenye hiyo Call Center na huuliza masuala ambayo hujibiwa moja kwa moja ” amesema Jaji Ngwembe.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here