Home BUSINESS TANZANIA KUTOAGIZA BARAKOA NJE YA NCHI

TANZANIA KUTOAGIZA BARAKOA NJE YA NCHI

Mkurugenzi Mkuu wa Boari ya Dawa- (MSD) Mavere Tukai akizungumza katika Semina ya Wahariri wa Vyombo vya habari inayofanyika kwa siku mbili April 5 hadi 6, 2023 Jijini Dodoma.

Mkurugenzi Mkuu wa Boari ya Dawa- MSD Mavere Tukai (kushoto) akisisitiza jambo alipokuwa akijibu maswali ya Wahariri wa Vyombo vya habari katika Semina hiyo Jijini Dodoma. (Kulia) ni, Mwenyekiti wa Semina hiyo Mgaya Kingoba. 

Meneja Mipango, Tathimini na Ufuatiliaji na MSD Hassan Ibrahim akitoa mada kuelezea Uwekezaji wa viwanda vya MSD katika siku ya pili ya Semina hiyo leo April 6,2023 Jijini Dodoma.

Mwenyekiti wa Jukwaa la Wahariri Tanzania (TEF) Deodatus Balile akitoa mada kuelezea umuhimu wa  wanahabari kuandika habari zinazolenga kutoa Elimu ya Afya kwa wananchi

Meneja Mawasiliano na Uhusiano wa MSD Bi.  Etty Kusiluka (kulia) akijadiliana jambo na Mwenyekiti wa (TEF) Deodatus Balile (kushoto) katika Semina hiyo.

Mkurugenzi Mkuu wa Boari ya Dawa- MSD Mavere Tukai (kushoto) akijadiliana jambo na Meneja Mawasiliano na Uhusiano wa Taasisi hiyo Bi. Etty Kusiluka (katikati) wakati wa Semina hiyo. (Kulia), ni Mwenyekiti wa Semina hiyo Mgaya Kingoba. 

(PICHA NA: HUGHES DUGILO)

DODOMA.

TANZANIA inatarajia kuondokana na kuagiza barakoa kutoka nje ya nchi baada ya kuanzisha viwanda vitakavyokuwa na jukumu la kutengeneza bidhaa hiyo muhimu nchini.

Aidha viwanda hivyo vitaisaidia Serikali kuokoa kiasi kikubwa cha fedha za kigeni kutokana na uwepo wa viwanda hivyo ambavyo tayari vimeshaanza kufanya kazi ya uzalishaji.

Hayo yameelezwa na Meneja Mipango, Tathimini na Ufuatiliaji na MSD Hassan Ibrahim katika Semina ya wahariri wa vyombo vya habari na Bohari ya Dawa (MSD) inayofanyika kwa siku mbili April 5 hadi 6 Jijini Dodoma.

Amesema kuwa kiwanda cha kutengeneza barakoa kipo Keko Jijini Dar es Salaam na kilianza uzalishaji Agosti mwaka 2020 lakini pia kuna kiwanda kingine cha barakoa aina ya N-95 ambacho kimezinduliwa mwezi Machi mwaka huu.

Kuhusu kiwanda cha mipira ya mikono kilichopo Idodi, Makambako mkoani Njombe kinaendelea vizuri na kimetengeneza ajira zaidi ya mia mbili za watanzania.

Ameeleza kuwa malighafi za kiwanda hicho cha kwanza katika Afrika Mashariki zinatoka Ifakara mkoani Morogoro, pamoja na Lushoto Mkoani Tanga.”Hadi kukamilika kwa kiwanda hicho kitagharimu zaidi ya shilingi bilioni 20.” 

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Jukwaa la Wahariri Tanzania (TEF), Deudetus Balile akizungumza alipokuwa akiwasilisha mada ya umuhimu wa vyombo vya habari katika masuala ya afya, ameupongeza uongozi wa MSD kwa kuwa karibu na vyombo vya habari ambao umewezesha mambo mbalimbali ya taasisi hiyo kujulikana.

“Pia naipongeza MSD kwa kuanzisha kiwanda cha mipira ya mikono kilichopo mkoani Njombe ambacho kitakuwa mkombozi kwa Tanzania kuacha kuagiza mipira hiyo ya mikono kutoka nje ya nchi,” amesema Balile.

Mwisho.

(PICHA MBALIMBALI ZA BAADHI YA WAHARIRI KATIKA SEMINA HIYO)

Previous articleMAGAZETI YA LEO ALHAMISI APRILI 6, 2023
Next articleWATUMISHI WANAOJITOLEA WAPEWE KIPAUMBELE – DKT. TULIA
Hughes Dugilo is a Writer, News Producer, Video-Photographer Journalist, and Video Editor experienced for 20 years now performing in News, Documentary, Advertisements and Television Programs. Aside from all above he own and operate his Blog known as Green Waves Media TZ since 2018.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here