Jeshi la Jadi Sungusungu wakitoa burudani kwenye Bonanza la Michezo likiongozwa na Kampeni ya Kataa Uhalifu Toa Taarifa Shinyanga Bila Uhalifu Inawezekana
Na Kadama Malunde – Malunde 1 blog
Jeshi la Polisi Mkoa wa Shinyanga kwa kushirikiana na wadau mbalimbali limeendesha ‘Kampeni ya Kataa Uhalifu Toa Taarifa Shinyanga Bila Uhalifu Inawezekana’ katika kata ya Chibe Manispaa ya Shinyanga ambayo ni miongoni mwa kata za kimkakati zinazopitiwa na Mradi wa Reli ya Mwendokasi (SGR).
Kampeni hiyo ya Kataa Uhalifu Toa Taarifa Shinyanga Bila Uhalifu Inawezekana imefanyika leo Jumamosi Aprili 15,2023 katika kata ya Chibe kupitia Bonanza la Michezo lililohudhuriwa na mamia ya wananchi ambapo mgeni rasmi alikuwa Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Mhe. Johari Samizi.
Bonanza hilo limehusisha utoaji elimu mbalimbali ikiwemo ya kukataa uhalifu na utoaji taarifa za uhalifu, ukatili wa kijinsia, huduma za kibenki, mashindano ya mbio za baiskeli kwa wanawake na wanaume, utoaji chanjo ya UVIKO 19, uchangiaji damu salama, ngoma, muziki, mchezo wa mpira wa miguu kati ya Radio Faraja Fm na Chibe Combine na burudani kadha kadha likiwemo onesho la Jeshi la Jadi Sungusungu kata ya Chibe.
Akizungumza wakati wa bonanza hilo, Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Mhe. Johari Samizi ametoa wito kwa wananchi kuepuka vitendo vya uhalifu na watoe taarifa za matukio ya uhalifu ikiwemo wanaohujumu mradi wa Reli ya Mwendokasi (SGR) unaopita katika kata hiyo ya Chibe.
“Mlinzi wa kwanza wa Mradi huu wa Reli ya Mwendokasi ni wananchi, tuulindeni mradi huu na tutoe taarifa za vitendo vya uhalifu katia jamii ili hatua ziweze kuchukuliwa”,amesema Mkuu huyo wa wilaya.
Mhe. Samizi ameikumbusha jamii kuhusu umuhimu wa uwabikaji wa kila mmoja katika kupiga vita mmomonyoko wa maadili katika jamii vinavyochochea matukio ya ulawiti na ubakaji akisema hayo yote yanatokea kutokana na kuwepo kwa mmomonyoko wa maadili katika jamii.
Aidha amesema vitendo vya ukatili wa kijinsia vinapaswa kupingwa na kila mmoja ili jamii iwe salama kwa ajili ya maendeleo nchini huku akisisitiza wazazi kulea watoto vizuri ili kuepuka wimbi la watoto wa mitaani.
Kwa upande wake Kamanda wa Polisi Mkoa wa Shinyanga ACP Janeth Magomi amewataka viongozi na wananchi washirikiane kutoa taarifa za uhalifu huku akikemea matukio ya baadhi ya wananchi kujichukulia sheria mkononi kushambulia watuhumiwa wa uhalifu.
“lli tupate taarifa za wahalifu na uhalifu ni lazima tuwe na taarifa, tunaomba sana wananchi mshirikiane na jeshi la polisi kuwafichua wahalifu katika jamii ikiwemo wanaofanya matukio ya ukatili wa kijinsia na kuhujumu Mradi wa Reli ya Mwendosi (SGR). Jeshi la Polisi linaamini Shinyanga bila uhalifu inawezekana”,ameeleza Kamanda Magomi.
Mratibu wa Kampeni, MC Amos Events maarufu MC Mzungu Mweusi amesema lengo la Kampeni ya Kataa Uhalifu Toa Taarifa Shinyanga Bila Uharifu Inawezekana ni kujenga uelewa kwa jamii kuhusu umuhimu wa kutoa taarifa za uhalifu katika jamii ambapo kata ya Chibe ni kata ya kimkakati kutokana na kwamba mradi wa Reli ya Mwendokasi unapita katika eneo hilo.
MC Mzungu Mweusi amewataja miongoni mwa wadau waliofanikisha kampeni hiyoWadhamini Benki ya CRDB, CJ Palace, Tigo, SBC Tanzania Limited, Haki Yangu Foundation, Miti Mirefu Dispensary, Diwani kata ya Chibe, Jeshi la Polisi, Mbunge wa Jimbo la Shinyanga Mjini Mhe. Patrobas Katambi, Soud Bakery, MC Mzungu Mweusi, Kamanda wa Jeshi la Polisi Shinyanga ACP Janeth Magomi, Malicha Microfinance, Juma Nkuba,TARURA, TANROADS, Mkurugenzi wa Manispaa ya Shinyanga, Jomaary Satura.
Katika michezo iliyofanyika washindi wameondoka na zawadi mbalimbali ambapo kwa upande wa mchezo wa mpira wa miguu Radio Faraja Fm wameondoka na zawadi ya Mbuzi na Kombe baada ya kuichapa Chibe Combine Fc bao 1-0 ambayo pia imeondoka na zawadi ya mbuzi mmoja.
Kwa upande wa mbio za baiskeli kwa wanawake waliozunguka uwanja wa mpita wa miguu mara 10 mshindi wa kwanza ni Temineta Charles aliyeondoka na zawadi ya shilingi 50,000/=, mshindi wa pili Grace Machiya shilingi 40,000/= ,mshindi wa tatu Happiness Ramadhani shilingi 30,000/=, mshindi wanne Dorcas Amosi shilingi 20,000/= na mshindi wa tano Elizabeth Hamis shilingi 10,000/= ambapo zawadi hizo zimetolewa na Shirika la Haki Yangu Foundation.
Kwa upande wa mbio za baiskeli kwa wanaume waliozunguka uwanja wa mpira wa miguu mara 50 mshindi wa kwanza ni Kulwa Jelard aliyeondoka na kitita cha shilingi 50,000/=, mshindi wa pili Masele Kichuya shilingi 40,000/= mshindi wa tatu Jelard Kondo shilingi 30,000/= mshindi wa nne Said Kulwa shilingi 20,000/= mshindi tano Wilson Malaika shilingi 10,000/= mshindi wa sita Mahona Kichuya shilingi 10,000/- mshindi wa saba sh. 10,000/= Shune Idasamaga shilingi 10,000/= mshindi wa nane Shija Said shilingi 10,000/= mshindi wa tisa Luhende Mzuzu sh 10,000/= na mshindi wa 10 Salum Clement shilingi 10,000/=.
Zawadi hizo kwa washindi wa mbio za baiskeli kundi la wanaume zimetolewa na Kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Shinyanga ACP Janeth Magomi.
ANGALIA PICHA HAPA CHINI
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Mhe. Johari Samizi akizungumza wakati wa Bonanza la Michezo likiongozwa na Kampeni ya Kataa Uhalifu Toa Taarifa Shinyanga Bila Uhalifu Inawezekana’ leo Aprili 15,2023 katika kata ya Chibe Manispaa ya Shinyanga. Picha zote na Kadama Malunde – Malunde 1 blog
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Mhe. Johari Samizi akizungumza wakati wa Bonanza la Michezo likiongozwa na Kampeni ya Kataa Uhalifu Toa Taarifa Shinyanga Bila Uhalifu Inawezekana’ leo Aprili 15,2023 katika kata ya Chibe Manispaa ya Shinyanga.
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Mhe. Johari Samizi akizungumza wakati wa Bonanza la Michezo likiongozwa na Kampeni ya Kataa Uhalifu Toa Taarifa Shinyanga Bila Uhalifu Inawezekana’ leo Aprili 15,2023 katika kata ya Chibe Manispaa ya Shinyanga.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Shinyanga ACP Janeth Magomi akizungumza wakati wa Bonanza la Michezo likiongozwa na Kampeni ya Kataa Uhalifu Toa Taarifa Shinyanga Bila Uhalifu Inawezekana’ leo Aprili 15,2023 katika kata ya Chibe Manispaa ya Shinyanga.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Shinyanga ACP Janeth Magomi akizungumza wakati wa Bonanza la Michezo likiongozwa na Kampeni ya Kataa Uhalifu Toa Taarifa Shinyanga Bila Uhalifu Inawezekana’ leo Aprili 15,2023 katika kata ya Chibe Manispaa ya Shinyanga.
Mratibu wa Kampeni, MC Amos Events maarufu MC Mzungu Mweusi akizungumza wakati wa Bonanza la Michezo likiongozwa na Kampeni ya Kataa Uhalifu Toa Taarifa Shinyanga Bila Uhalifu Inawezekana’ leo Aprili 15,2023 katika kata ya Chibe Manispaa ya Shinyanga.
Mratibu wa Kampeni, MC Amos Events maarufu MC Mzungu Mweusi akizungumza wakati wa Bonanza la Michezo likiongozwa na Kampeni ya Kataa Uhalifu Toa Taarifa Shinyanga Bila Uhalifu Inawezekana’ leo Aprili 15,2023 katika kata ya Chibe Manispaa ya Shinyanga. Kushoto ni Polisi Kata ya Chibe, Mkaguzi Msaidizi wa Polisi Issa Mnafi.
Mkuu wa Dawati la Jinsia Mkoa wa Shinyanga SSP Monica Sehere ambaye ni Polisi Jamii Mkoa wa Shinyanga akizungumza wakati wa Bonanza la Michezo likiongozwa na Kampeni ya Kataa Uhalifu Toa Taarifa Shinyanga Bila Uhalifu Inawezekana’ leo Aprili 15,2023 katika kata ya Chibe Manispaa ya Shinyanga.
Afisa biashara Benki ya CRDB tawi la Shinyanga, Mwanahamisi Iddy akizungumza wakati wa Bonanza la Michezo likiongozwa na Kampeni ya Kataa Uhalifu Toa Taarifa Shinyanga Bila Uhalifu Inawezekana’ leo Aprili 15,2023 katika kata ya Chibe Manispaa ya Shinyanga.
Afisa Programu wa Shirika la Haki Yangu Foundation, Christa Christian akizungumza wakati wa Bonanza la Michezo likiongozwa na Kampeni ya Kataa Uhalifu Toa Taarifa Shinyanga Bila Uhalifu Inawezekana’ leo Aprili 15,2023 katika kata ya Chibe Manispaa ya Shinyanga.
Afisa Maendeleo ya jamii mkoa wa Shinyanga Tedson Ngwale akizungumza wakati wa Bonanza la Michezo likiongozwa na Kampeni ya Kataa Uhalifu Toa Taarifa Shinyanga Bila Uhalifu Inawezekana’ leo Aprili 15,2023 katika kata ya Chibe Manispaa ya Shinyanga.
Diwani wa kata ya Chibe John Kisandu akizungumza wakati wa Bonanza la Michezo likiongozwa na Kampeni ya Kataa Uhalifu Toa Taarifa Shinyanga Bila Uhalifu Inawezekana’ leo Aprili 15,2023 katika kata ya Chibe Manispaa ya Shinyanga.
Afisa Mtendaji kata ya Chibe, Ponsian Ngodita akizungumza wakati wa Bonanza la Michezo likiongozwa na Kampeni ya Kataa Uhalifu Toa Taarifa Shinyanga Bila Uhalifu Inawezekana’ leo Aprili 15,2023 katika kata ya Chibe Manispaa ya Shinyanga.
Mratibu wa kitaifa wa Shirika la Haki Yangu Foundation Francis Chiduo (kushoto) na Afisa Programu wa Shirika la Haki Yangu Foundation, Christa Christian wakigawa vipeperushi wakati wa Bonanza la Michezo likiongozwa na Kampeni ya Kataa Uhalifu Toa Taarifa Shinyanga Bila Uhalifu Inawezekana’ leo Aprili 15,2023 katika kata ya Chibe Manispaa ya Shinyanga.
Mratibu wa kitaifa wa Shirika la Haki Yangu Foundation Francis Chiduo akigawa vipeperushi wakati wa Bonanza la Michezo likiongozwa na Kampeni ya Kataa Uhalifu Toa Taarifa Shinyanga Bila Uhalifu Inawezekana
Burudani ya ngoma ikiendelea kwenye Bonanza la Michezo likiongozwa na Kampeni ya Kataa Uhalifu Toa Taarifa Shinyanga Bila Uhalifu Inawezekana
Wananchi wakiwa kwenye Bonanza la Michezo likiongozwa na Kampeni ya Kataa Uhalifu Toa Taarifa Shinyanga Bila Uhalifu Inawezekana
Jeshi la Jadi Sungusungu wakitoa burudani kwenye Bonanza la Michezo likiongozwa na Kampeni ya Kataa Uhalifu Toa Taarifa Shinyanga Bila Uhalifu Inawezekana
Jeshi la Jadi Sungusungu wakitoa burudani kwenye Bonanza la Michezo likiongozwa na Kampeni ya Kataa Uhalifu Toa Taarifa Shinyanga Bila Uhalifu Inawezekana
Jeshi la Jadi Sungusungu wakitoa burudani kwenye Bonanza la Michezo likiongozwa na Kampeni ya Kataa Uhalifu Toa Taarifa Shinyanga Bila Uhalifu Inawezekana
Burudani ikiendelea kwenye Bonanza la Michezo likiongozwa na Kampeni ya Kataa Uhalifu Toa Taarifa Shinyanga Bila Uhalifu Inawezekana
Zoezi la uchangiaji damu salama likiendelea Bonanza la Michezo likiongozwa na Kampeni ya Kataa Uhalifu Toa Taarifa Shinyanga Bila Uhalifu Inawezekana
Mbio za baiskeli zikiendelea kwenye Bonanza la Michezo likiongozwa na Kampeni ya Kataa Uhalifu Toa Taarifa Shinyanga Bila Uhalifu Inawezekana
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Mhe. Johari Samizi akikagua timu za mpira wa miguu wakati wa Bonanza la Michezo
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Mhe. Johari Samizi akikagua timu za mpira wa miguu wakati wa Bonanza la Michezo
Mbio za baiskeli zikiendelea kwenye Bonanza la Michezo likiongozwa na Kampeni ya Kataa Uhalifu Toa Taarifa Shinyanga Bila Uhalifu Inawezekana
Mechi kati ya Chibe Combine (jezi ya bluu) dhidi ya Radio Faraja Fm ikiendelea
Mechi kati ya Chibe Combine (jezi ya bluu) dhidi ya Radio Faraja Fm ikiendelea
Mbio za baiskeli kundi la wanawake zikiendelea
Mshindi Mbio za baiskeli kundi la wanawake Temineta Charles akiendelea na mbio
Mshindi Mbio za baiskeli kundi la wanawake Temineta Charles
Bonanza linaendelea
Bonanza linaendelea
Bonanza linaendelea
Bonanza linaendelea
Bonanza linaendelea
Bonanza linaendelea
Bonanza linaendelea
Bonanza linaendelea
Bonanza linaendelea
Bonanza linaendelea
Burudani ikiendelea wakati wa Bonanza la Michezo
Mkazi wa Chibe akizungumza wakati wa Bonanza la Michezo
Mkazi wa Chibe akizungumza wakati wa Bonanza la Michezo
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Mhe. Johari Samizi akimkabidhi zawadi mshindi wa kwanza mbio za baiskeli wanaume Kulwa Jelard
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Mhe. Johari Samizi akimkabidhi zawadi ya mbuzi kwa timu ya Chibe Combine
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Mhe. Johari Samizi akimkabidhi zawadi ya mbuzi kwa timu ya Radio Faraja
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Mhe. Johari Samizi akimkabidhi zawadi ya Kombe kwa timu ya Radio Faraja
[4/15, 9:02 PM] +255 688 405 951: