GAVANA wa Benki Kuu ya Tanzania, Bw. Emmanuel Tutuba.
Imam wa Msikiti wa Maamour Upanga jijini Dar es Salaam, Sheikh Issa Othman (Mufti London),
Wageni waalikwa
Picha ya pamoja
(Picha zote na BoT).
Na: Khalfan Said, DAR ES SALAAM
GAVANA wa Benki Kuu ya Tanzania, Bw. Emmanuel Tutuba amewahimiza Watanzania kuchapa kazi kwa bidii ili kuongeza uzalishaji na hivyo kukuza uchumi.
Bw. Tutuba ameyasema hayo katika hafla ya futari aliyowaandalia viongozi wa Serikali, Jumuiya ya wenye Mabenki, Watoto wa Madrasa na Makundi Maalum kwenye Makao Makuu ndogo ya BoT jijini Dar es Salaam Aprili 20, 2023.
“Sisi kama Benki Kuu tunaendelea kusimamia uchumi wa nchi yetu na niwahakikishie uchumi wetu uko imara, mfumuko wa bei umedhibitiwa na fedha yetu pia iko imara, sekta ya fedha inazidi kukua.” Alisema Bw. Tutuba na kuongeza .“Ninachoomba kutoka kwenu ni ushirikiano, tufanye kazi kwa bidii ili tuzalishe zaidi kwani hiyo ni nyenzo muhimu katika kujenga uchumi imara.” Alifafanua.
Gavana huyo wa BoT alisema Benki Kuu ya Tanzania kwa umakini mkubwa itaendelea kusimamia ustahimilivu wa uchumi, sera ya fedha, mfumuko wa bei,utoaji wa leseni kwenye taasisi za fedha, udhibiti sekta ya fedha na usimamizi wa mauzo ya nje.
“Juzi nilikuwa kwenye Mikutano ya Benki ya Dunia (WB) wameisifu nchi yetu kwa usimamizi mzuri wa uchumi ikilinganishwa na Mataifa mengine.” Alidokeza.
Aidha Gavana Tutuba aliwashukuru wote walioitikia mwaliko wa BoT kuja kujumuika na watumishi wa Benki hiyo katika sadaka hiyo ya futari.
Tukio kama hili tunalifanya kwenye matawi yetu yote Saba (7) na lengo kwakweli ni kuungana na jamii katika kufanya matendo mema yanayompendeza Mungu.
“Kufunga, kusali kutoa sadaka ni mambo ambayo Mwenyezimungu huyapokea kwa haraka.” Alisema Bw. Tutuba.
Awali akitoa Mawaidha kuhusu “Uislamu na Uchumi” kabla ya futari, Imam wa Msikiti wa Maamour Upanga jijini Dar es Salaam, Sheikh Issa Othman (Mufti London), alisema ipo misingi sita (6) inayoelezea Uislamu na Uchumi ambayo ni udugu, Naswiha, kuheshumu makubaliano, Hofu ya Mungu, na huruma.
Sheikh Othman pia alisema, Nidhamu ni jambo muhimu sana katika Uislamu.
Funga ya Mwezi Mtukufu wa Radhan, inajenga nidhamu binafsi mambo ambayo yanahimizwa katika uislamu.
Akifafanua alisema, Nidhamu hiyo imegawanyika katika sehemu tatu ambazo ni active diceplin, reactive dicepli (inafundisha ustahikilivu kwamba hata unapochokozwa hupaswi kujibiza na mwisho ni proactive deciplin (mambo ambayo umeyazingatia au kuyafuata wakati wa Mfungo wa Mwezi Mtukufu wa Ramadhani uendelee kuyafuata hata baada ya kumalizika kwa Mfungo.
Naye Sheikh Muharram Mziwanda aliwahimiza Watanzania kwa ujumla kuendelea kuenzi Amani na Utulivu nchini kwani mafanikio ya kukua kwa uchumi yanategemea sana hali ya Amani na Utulivu wa nchi.
“Uchumi hauwezi kusogea ikiwa Msingi wa uchumi haupo (utulivu), tuhakikishe tunaendelea kuenzi Amani na Utulivu kila mmoja kwenye nafasi zetu,” alisema Sheikh Mziwanda.
Credit – K-VIS BLOG.