Home LOCAL DC JOKATE AWAOMBA VIONGOZI WA DINI KUENDELEA KUIOMBEA SERIKALI

DC JOKATE AWAOMBA VIONGOZI WA DINI KUENDELEA KUIOMBEA SERIKALI

Na: Miko Luoga Tanga

Mkuu wa wilaya ya Korogwe mkoani Tanga Mhe, Jokate Mwegelo amewaomba viongozi wa dini na waumini wilayani humo kuwaombea viongozi wa serikali na ardhi ya Tanzania ili Taifa liendelee kuwa salama.

Mhe, Jokate amesema hayo leo jumapili Aprili 16, 2023 katika ibada ya shukurani ya kutimiza miaka 20 ya huduma ya kwaya ya Maranatha iliyofanyika kwenye Kanisa Anglikana mtakatifu Andrea Manundu Korogwe.

Katika Ibada hiyo iliyoambatana na kuchangia mfuko wa kununua gari ya kwaya hiyo mhe, Jokate alimwakilisha mkuu wa mkoa wa Tanga Mhe, Waziri Kindamba na kutoa salamu za Serikali kwa niaba yake.

Aidha amewaeleza waimbaji wa kwaya hiyo na waumini walioshiriki kuwa Mkuu wa Mkoa wa Tanga Mhe, Waziri kindamba ameahidi kuchangia mfuko huo kiasi cha shilingi milioni tano naye akiahidi kuunga mkono zoezi hilo kiasi cha shilingi milioni tatu.

Hatahivyo Kanisa Anglikana Mtakatifu Andrea Korogwe limefanya ibada maalumu ya kumuombea Mkuu wa Wilaya ya Korogwe Mhe, Jokate Mwegelo ili aweze kutekeleza vyema majukumu yake.

Kasisi Canon Dominic Singano kutoka Kanisa Anglikana mtakatifu Andrea Magomeni Dar es Salaam amewatia moyo wa matumaini waumini na waimbaji kuwa wakiungana zoezi la ununuzi wa gari hilo litakamilika kwa wakati ili injili ya Kristo ihubiriwe kote nchini.

Kwa upande wake Kasisi kiongozi wa mtaa wa Mtakatifu Andrea Manundu Korogwe Canon Aidan Kamote amesema waumini wa Kanisa hilo wameendelea kuunga mkono matukio yote ya kwaya zinazohudumu kanisani hapo ili ziweze kutimiza malengo husika.

Zoezi la kuchangia mfuko wa ununuzi wa Gari la Kwaya ya Maranatha jumla ya fedha taslimu za kitanzania Shilingi cha 4,500,000 zimepatikana na ahadi zikiwa milioni 17,400,000 nakwamba zoezi hilo ni endelevu ili kufikia lengo la kukusanya 70, 000,000/-

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here