Home BUSINESS CHUO KIKUU CHA SAYANSI NA TEKNOLOJIA MBEYA WAKUMBUSHWA KUSAJILI BUNIFU ZAO

CHUO KIKUU CHA SAYANSI NA TEKNOLOJIA MBEYA WAKUMBUSHWA KUSAJILI BUNIFU ZAO

Baadhi ya wahadhiri na Wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Sayansi na Teknolojia Mbeya (MUST), wamekumbushwa kulinda Bunifu zao Wakala wa Usajili wa Biashara na Leseni (BRELA), ili ziwanufaishe.

Kauli hiyo imetolewa na Afisa Sheria kutoka BRELA Bw. Abdulkarim Nzori wakati wa mafunzo chuoni hapo Aprili 19, 2023. Mafunzo hayo yanalenga kuwajengea uwezo Wahadhiri pamoja na Wanafunzi kuhusu masuala ya Miliki Ubunifu.

Amesema kuwa Chuo cha Sayansi na Teknolojia kinakuwa na tafiti mbalimbali ambazo matokeo yake kwa namna moja yanaweza kufanyiwa mchakato wa kuwa bidhaa au namna za kutengeneza vitu mbalimbali hivyo, wakilinda vumbuzi hizo zitakuwa na manufaa kwao binafsi na kwa jamii pia.

Ameongeza kwa mifano kuwa haki za Miliki Ubunifu ikiwemo Hataza na Alama za Biashara na Huduma zimekuwa na thamani ulimwenguni hivyo Bunifu wanazo zianzisha au zibuni wazisajili BRELA ili viwanufaishe na zisaidie jamii.

Awali akitoa neno la Ufunguzi Kaimu Makamu Mkuu wa Chuo Elimu, Tafiti na Ushauri, Prof. Godliving Mtui amewapongeza BRELA kwa kuandaa mafunzo hayo ya Miliki Ubunifu na kufika katika Chuo hicho ambacho moja kwa moja kinajihusisha katika masuala ya Sayansi na Teknolojia.

Pia amewataka BRELA kuendelea kufika katika chuo hicho pale wanapopewa mialiko na kutoa mafunzo kuhusu huduma zinazotolewa na BRELA.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here