Home LOCAL BIBI WA MIAKA 70 AUWAWA AKITUHUMIWA KWA UCHAWI GEITA.

BIBI WA MIAKA 70 AUWAWA AKITUHUMIWA KWA UCHAWI GEITA.

Bibi mmoja Mwenye umri wa Maika 70 Mkazi wa kijiji cha Mwenegezi kata ya Nyakagomba wilaya ya Geita Mkoani Geita ambae Jina lake mpaka sasa halijafahamika ameuwawa kwa kukatwa na kitu chenye ncha kali kichwani.

Akithibitisha kutokea kwa tukio hilo Kaimu Kamanda wa jeshi la Polisi Mkoa wa Geita Kamishina Msaidizi wa Polisi Berthaneema Mlay Amesema bibi hayu ameuwawa na watu wasio julikana akituhumiwa Kujihusisha na imani za kishirikina.

Kamanda Mlay amesema mpaka sasa jeshi hilo la polisi linawashikilia Watu sita wakiwemo wanawake wawili pamoja na wanaume wa nne kwa ajili ya uchunguzi kwa lengo la kubaini chanzo halisi cha tukio hilo.

Amewataka wakazi wa mkoa wa Geita kuachana na imani za kishirikina kutokana na kuwepo na matukio ya watu wengi kuuwawa wakituhumiwa kujihusha na imani za kishirikina.

Amesema watu hao sita waliokamatwa jeshi hilo litahakikisha linafanya uchunguzi kwa kina ili kubaini wale wote waliohusika na tukio hilo watachukuliwa hatua kali kwa mjibu wa sheria.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here