Home Uncategorized BALOZI MBAROUK ASHIRIKI SIKU YA UHURU WA AFRIKA KUSINI AITA WAWEKEZAJI WAKE...

BALOZI MBAROUK ASHIRIKI SIKU YA UHURU WA AFRIKA KUSINI AITA WAWEKEZAJI WAKE NCHINI

Naibu Waziri Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Balozi Mbarouk Nassor Mbarouk (wa tatu kulia) aliposhiriki maadhimisho ya miaka 29 ya Uhuru wa Jamhuri ya Afrika Kusini yaliyofanyika jijini Dar es Salaam

Naibu Waziri Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Balozi Mbarouk Nassor Mbarouk akizungumza katika maadhimisho ya miaka 29 ya Uhuru wa Jamhuri ya Afrika Kusini yaliyofanyika jijini Dar es Salaam.

Naibu Waziri Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Balozi Mbarouk Nassor Mbarouk akiongoza wanadiplomasia waliohudhuria  maadhimisho ya miaka 29 ya Uhuru wa Jamhuri ya Afrika Kusini kukata keki malum kwa ajili ya maadhimisho hayo yaliyofanyika jijini Dar es Salaam

Naibu Waziri Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Mbarouk Nassor Mbarouk akiwa na waheshimiwa Mabalozi kutoka nchi mbalimbali wanaowakilisha nchi zao nchini waliposhiriki  maadhimisho ya miaka 29 ya Uhuru wa Jamhuri ya Afrika Kusini yaliyofanyika jijini Dar es Salaam

Naibu Waziri Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Mbarouk Nassor Mbarouk akisalimiana na  Balozi Mstaafu Mhe. Getrude Mongela walipokutana katika maadhimisho ya miaka 29 ya Uhuru wa Jamhuri ya Afrika Kusini yaliyofanyika jijini Dar es Salaam

Naibu Waziri Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Balozi Mbarouk Nassor Mbarouk (Mb.) ameshiriki sherehe za maadhimisho ya miaka 29 ya Uhuru wa Jamhuri ya Afrika Kusini zilizofanyika jijini Dar es Salaam na kuwaita wawekezaji wengi zaidi waje kuwekeza nchini.

Akizungumza katika hafla hiyo Mhe. Balozi Mbarouk amesema Tanzania itaendelea kushirikiana na Afrika Kusini kuendelea kuuenzi uhusiano wa kidugu na wa kihistoria uliopo kati ya nchi hizo ambao uliasisiwa na viongozi waasisi wa mataifa hayo.

“Tanzania itaendelea kutumia fursa za uwekezaji zinazopatikana nchini Afrika Kusini na nitoe  wito kwa wawekezaji wengi zaidi wa Afrika Kusini waje Tanzabia kuwekeza hasa ikizingatia kuna fursa katika maeneo ya kilimo, uzalishaji, mifugo, viwanda vya dawa, usafiri, utalii, madini na viwanda vya kusindika mazao ya chakula,”alisema.

Amesema wakati Taifa la Afrika Kusini likiadhimisha siku ya uhuru wake Tanzania itaendelea kushirikiana na Afrika Kusini ili kuhakikisha nchi zote zinanufaika na uwepo wa uhusiano huo.

Amesema ushirikiano mzuri uliopo kati ya Tanzania na Afrika Kusini umeoneshwa zaidi na ziara ya kitaifa aliyoifanya nchini Afrika Kusini Rais wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan pamoja na kufanyika kwa  mikutano ya pamoja kati ya nchi hizi.

Akizungumza katika  hafla hiyo Balozi wa Afrika Kusini nchini Mhe. Noluthando Mayende- Malepe amesema Afrika Kusini inajali na kuthamini mchango mkubwa ambao Tanzania imetoa katika harakati za ukombozi wa nchi hiyo na kuifanya Tanzania kuwa nyumbani kwa wapigania uhuru wa Afrika Kusini.

“Tunaishukuru sana serikali na wananchi wa Tanzania kwa mambo yote ambayo Tanzania imeifanyia Afrika Kusini  wakati wote hadi kufikia kupata uhuru wetu, kwakweli sisi tunawashukuru sana, niwahakikishie kuwa Afrika Kusini itaendelea kuuthamini mchango wenu katika uhuru wetu na tutaendelea kuuenzi uhusiano wa kidugu na wa kihistoria uliopo kati ya nchi zetu mbili hizi, alisema.

Ameahidi kuwa Tanzania na Afrika Kusini zitaendelea kushirikiana katika mambo mengi ambayo nchi mbili hizi zimekuwa zikiyafanya.

Hafla hiyo ilihudhuriwa na waheshimiwa Mabalozi na Wakuu wa Mashirika ya Kimataifa wanaoziwakilisha nchi zao hapa nchini

Previous articleGGML YAIBUKA MSHINDI WA JUMLA MUONESHAJI BORA KATIKA MAONESHO YA AFYA NA USALAMA MAHALI PA KAZI 2023
Next articleTAASISI ZA SERIKALI ZIANDAE MIKAKATI YA KUTATUA CHANGAMOTO ZINAZOIBULIWA KWENYE MIJADALA – DKT. ASHIL
Hughes Dugilo is a Writer, News Producer, Video-Photographer Journalist, and Video Editor experienced for 20 years now performing in News, Documentary, Advertisements and Television Programs. Aside from all above he own and operate his Blog known as Green Waves Media TZ since 2018.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here