Na: Mwandishi wetu
KATIKA kukamilisha mfungo wa mwezi mtukufu wa ramadhani Shirika la ndege la Emirates,inatarajia kuadhimisha tukio la aina yake la ladha za kikanda ndani ya ndege, vyakula vya kitamaduni vya sikukuu ya Eid El Fitri kwenye vyumba vya mapumziko na filamu mpya za kiarabu.
Taarifa iliyotolewa kwa vyombo vya habari jana jijini Dar es Salaam,imesema tukio hilo linatarajia kufanyika Aprili 21 hadi 24 mwaka huu, abiria wa daraja la uchumi wanaotoka Dubai watahudumiwa na ladha pendwa za Eid ikiwemo vyakula vya aina mbalimbali.
Imesema abiria wanaosafiri katika daraja la uchumi wa hali ya juu, Biashara na daraja la kwanza,wao nao wataweza kufurahia radha ya vyakula mbalimbali vipya ili kuwafanya wateja wao kufurahia huduma zinazotolewa na shirika hilo kipindi hicho cha sikukuu.
”Emirates itawapa abiria mlo mtamu kutokana na kushurekea sikukuu ya Eid El Fitri ambapo Waislamu duniani kote wamefunga mwezi mmoja,hivyo tumeamua kuleta vyakula vitamu ambavyo wateja wetu watafurahia,” mesema na kuongeza.
”Mbali na vyakula hivyo pia shirika hilo limejipanga kuboresha vyumba vya mapumziko katika kuwaboreshea mazingira yenye madhari nzuri pamoja na vinywaji vitakavyokuwa vya ubora wake,”imesema.
Aidha imesema ,maudhui mbalimbali yatapatikana kwenye burudani ambazo zimeshinda tuzo ya upeperushaji wa barafu kwa wale wanaosafiri kipindi cha Eid al Fitr, ikiwa ni pamoja na kutazama zaidi ya filamu 100 za kiarabu ikiwa ni pamoja na matoleo mapya.