Home BUSINESS MWONEKANO MPYA NGORONGORO WAVUTIA

MWONEKANO MPYA NGORONGORO WAVUTIA

•Uoto wa asili, ikolojia vyaanza kurudi kwa kasi katika maeneo yaliyohamwa na wakazi

•Matumaini yazidi kuwa makubwa,

•Wadau watoa Ushauri

Baada ya baadhi ya wakazi wa maeneo ya Ngorongoro kuhamia Msomera Mkoani Tanga, Ikolojia na uoto wa asili vimenza kuejea kwa katika maeneo waliyobomoa makazi yao jambo linaloonyesha tija kubwa ya zoezi la Uhamaji Kwa hiyari

Wanahabari na wadau wa Kituo cha wanahabari watetezi wa Rasilimali na Taarifa (Mecira) Veronica Mheta na Dixon Busagaga walijionea mabadiliko makubwa tena ya muda mfupi walipotembelea kwenye baadhi ya zilipokuwa ambazo wamiliki wake waliamua kuhama Kwa hiyari kuhamia Msomera na kwengineko, maeneo hayo ni kwa aliyekuwa Mbunge wa Ngorongoro,Saning’o ole Telele na kwa Foible Lukumay wakazi wa kata ya Enduleni wilayani Ngorongoro na kwengineko katika eneo hilo .

“Kwa macho yangu nilijionea namna eneo hili lilivyokuwa limeathirika. Lakini Leo ninafurahi kuona ikolojia na uoto wa asili vimeanza kurejea kwa kasi kubwa sana” Amenukuliwa Mheta

“Nimeambiwa kuwa hapa pataota hata miti iliyokuweko awali na ikakatwa na wakazi waliokuwa wakiushi Ili kujenga Nyumba na maboma ya mifugo, Kwa kweli kuna tija kubwa sana kwenye zoezi la Uhamaji wa hiyari”. Aliongeza Busagaga.

Miongoni mwa Sababu zilizopelekea wadau wa mazingira na watetezi wa haki za binaadamu kupaza sauti na kuitaka Serikali kutafuta utaratibu mpya wa kufanya Ngorongoro kuwa sehemu Salama kwa ajili ya Wanyama, Mifugo na binaadamu ni pamoja na;-

1.ONGEZEKO KUBWA LA WATU ambapo awali kulikuwa na Watu wasiozidi 8000 lakini sasa hivi wapo zaidi ya watu 120,000

2. ONGEZEKO KUBWA LA MIFUGO ambapo awali ilikuwa chini ya 50,000 lakini sasa hivi imevuka 1.1m

3. Miripuko ya magonjwa Kutokana na kuingiliana kulikopitiliza baina ya wanadamu, Wanyama na mifugo

4. Umasikini uliopitiliza ambapo ni asilimia 3 pekee ndio wanamiliki asilimia 80 ya mifugo yote 1.1m na hivyo kuwafanya wananchi MANAMBA

5. Kutokujua kusoma na kuandika ambapo zaidi ya asilimia 63 ya Wananchi wa Ngorongoro HAWAJUI KUSOMA NA KUANDIKA

6. Ongezeko kubwa sana la makazi(Nyumba) zisizoruhusiwa kisheria kujengwa hifadhini sambamba na ufungaji wa mitambo, umeme wa sola, nakadharika.

Hivyo kuifanya Serikali kuchukua hatua ya kuruhusu zoezi la Uhamaji wa hiyari kutoka hifadhini humo kwenda Msomera kwa atakayependa na kokote kule atakayetaka mtu anayehama yeye pamoja na mali zake zote ikiwemo mifugo.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here