Home LOCAL ZIARA YA CHONGOLO IKUNGI

ZIARA YA CHONGOLO IKUNGI

Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi Ndugu Daniel Chongolo akimsikiliza Mwenyekiti wa shina namba 13 Ndugu Marita Ambrosi Makhwele wakati wa kikao maalum cha shina hilo lililopo Uliyampiti wilaya ya Ikungi mkoani Singida.

Wengine pichani ni Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi CCM Taifa Ndugu Sophia Mjema (kushoto), Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Singida Ndugu Martha Mlata na Katibu wa Shina hilo Maria Edward Henku (kulia).

Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi Ndugu Daniel Chongolo akizungumza na wakazi wa shina namba 13 wakati wa kikao maalum cha shina hilo lililopo Uliyampiti wilaya ya Ikungi mkoani Singida.

Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi Ndugu Daniel Chongolo akipata maelezo juu ya maendeleo ya ujenzi wa Chuo cha Ufundi Stadi (VETA) cha Ikungi kutoka kwa Mkurugenzi wa VETA kanda ya kati Ndugu John Mwanja (kulia)

 Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi Ndugu Daniel Chongolo akiupata maelezo juu ya vifaa tiba vya kisasa vilivyowekwa katika Hospitali ya Wilaya ya Ikungi mkoani Singida.

Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi Ndugu Daniel Chongolo akiwasabahi wananchi walifika kupata huduma katika hospitali ya wilaya ya Ikungi mkoani Singida.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here