Home BUSINESS WCF YAJIDHATITI KUBAINI UDANGANYIFU

WCF YAJIDHATITI KUBAINI UDANGANYIFU

Mkurugezi wa Tathimini wa Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi (WCF) Dkt. Abdullssalaam Omar akizungumza alipokuwa akitoa mada ya Tathimini za Madai kwa watumishi wanaopata madhara wakiwa kazini, wakati wa Kikao kazi kati ya Mfuko huo na Jukwaa la Wahariri Tanzania (TEF) kilichofanyika leo Machi 20, 2023 Bagamoyo Mkoani Pwani.

Mkurugenzi Mkuu wa mfuko wa Fidia kwa wafanyakazi (WCF) Dkt John Mduma (kulia), pamoja na Mwenyeti wa Jukwaa la Waariri Tanzania – TEF, Deodatus Balile (kusoto), wakipiga makofi wakati wakisiliza mada iliyokuwa ikitolewa na Dkt. Abdulssalaam Omar katika kikao kazi hicho.

Afisa Mtendaji Mkuu wa TEF, Bi. Anitha Mendoza akifuatilia mada ya Tathimini za Madai iliyotolewa na Dkt. Abdulssalaam Omar kwenye Kikao kazi hicho.

(PICHA NA: HUGHES DUGILO)

Na: Hughes Dugilo, BAGAMOYO

Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi (WCF), umeeleza kuja na Mpango thabiti utakaozuia udanganyifu uliokuwa unafanywa na baadhi ya watumishi wake wasio waaminifu ambapo hutengeneza ajali ama maradhi ili kunufaika na mafao yanayotolewa na mfuko huo kwa mtumishi anapopata na changamoto hizo awapo kazini.

Kauli hiyo imetolewa leo  Machi 20,2023 Mjini Bagamoyo mkoani Pwani na Mkurugenzi wa huduma za tathmini wa Mfuko wa WCF, Dkt Abdulsalaam Omar wakati akielezea hali ya tathamini ya madai kwa wanufaika wa Mfuko huo.

Dkt Omar amesema kuwa hapo awali baadhi ya watumishi walikuwa wanasababisha mfuko huo kupata hasara kwa kuingiza madai ambayo hayana ukweli kwa kutengeneza ajali ili kujipatia fedha zinazotokana na mafao yasiyowahusu kupitia mfuko huo.

“Lakini sasa baada ya kuja na mfumo maalumu wa kufuatilia au kufanya tathmini tumekuwa tukibaini udanganyifu unaofanywa ili kujipatia tu fedha za madai” amesema Dkt Omar.

Awali Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Fidia kwa wafanyakazi (WCF) Dkt. John Mduma, ameshukuru uongozi wa Rais Dkt Samia Suluhu Hassan kwa kuuwezesha mfuko huo kutimiza majukumu yake katika kuhakikisha  unawafikia wananchi wengi na kwa wakati.

“Katika kipindi hiki cha Awamu ya Sita inayoongozwa na Rais Dkt Samia Suluhu Hassan Sekta Binafsi kwa Sasa inachangia Asilimia 05. Ikishuka kutoka Asilimia 1 iliyokuwa ikichangia hapo awali” amesema Dkt Mduma.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here