Home LOCAL WAZIRI UMMY ATEMBELEA WATUMISHI WALIOWEKWA KARANTINI

WAZIRI UMMY ATEMBELEA WATUMISHI WALIOWEKWA KARANTINI

 Na: WAF – Bukoba, Kagera

Waziri wa Afya Mhe. Ummy Mwalimu amewatembelea watumishi wa afya waliowekwa sehemu maalumu ya uangalizi baada ya kuwahudumia wagonjwa wa Marburg walioripotiwa katila Wilaya ya Bukoba Mkoani Kagera.

Ziara hiyo ameifanya leo akiambatana na Wawakilishi kutoka Shirika la Afya Duniani (WHO) Dkt. Zabron Yoti na Shirika la Kuhudumia Watoto Duniani (UNICEF) Bi. Shalini Bahuguna baada ya kutembelea katika Vijiji vya Kata ya Maluku na Kanyangele ambapo ugonjwa huo umeanzia

Waziri Ummy amewatia moyo watumishi hao kwakuwa Serikali ipo pamoja nao na lengo ni kuendelea kuwalinda wao na wanaowazunguka ikiwemo familia zao.

“Niwatie moyo ndugu zangu huu ugonjwa utaisha kwakuwa Serikali imedhamiria kuendelea kupambana ili kutokomeza kabisa na hali itarudi kama zamani.

Mwisho, Waziri Ummy amewataka watumishi hao wa Afya kuzingatia Kanuni na Taratibu za Udhibiti wa Maambukizi (Infection Prevention and Control) wakati wote wanapowahudumia wagonjwa.

Previous articleKAGERA NI SHWARI HAKUNA MAAMBUKIZI MAPYA YA UGONJWA WA MARBURG
Next articleMAMA SALMA KIKWETE AIPONGEZA OREXY GAS TANZANIA KWA KUGAWA MITUNGI 100 YA GESI KWA WAKIMAMA JIJINI DAR
Hughes Dugilo is a Writer, News Producer, Video-Photographer Journalist, and Video Editor experienced for 20 years now performing in News, Documentary, Advertisements and Television Programs. Aside from all above he own and operate his Blog known as Green Waves Media TZ since 2018.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here